Ruzuku yashusha bei ya Diezel,Petrol na mafuta ya taa Kenya

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa Uhuru Kenyatta ameidhinisha nyongeza ya ruzuku ya shilingi bilioni 16.675 ili kuendelea kuwapunguzia makali ya bei za mafuta wananchi nchini humo.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Julai 14, 2022 na Msemaji wa Ofisi ya Rais Ikulu ya Kenya, Kanze Dena Mararo.

"Niwaarifu kwamba, Mheshimiwa Rais leo ameidhinisha nyongeza ya ruzuku ya shilingi za Kenya bilioni 16.675 ili kuwapunguzia Wakenya makali katika ongezeko la bei za mafuta.

"Kwa hatua ya leo ya Rais, mafuta ya Diesel yataendelea kwa bei ya reja reja kuuzwa shilingi 140.00, Petrol kwa shilingi 159.12 na mafuta ya taa kwa shilingi 127.94, bila serikali kuingilia kati bei ya mafuta kwa lita ya Diezel ingeuzwa shilingi 193.64, Petrol shilingi 209.95 na mafuta ya taa shilingi 181.13 kwa lita;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news