Serikali imedhamiria kuiona Tanzania inakuwa lango la uchumi Afrika-Prof.Kahyarara

NA MWANDISHI WETU

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Prof. Godius Kahyarara amesema Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria kuiona Tanzania inakuwa lango la Uchumi wa Bara la Afrika kwa kuwa na Viwanda vikubwa ambavyo vitasaidia kupeleka Bidhaa kwenye Soko la Afrika kuongeza ajira na pato la Taifa.
Prof. Kahyarara pia amewakaribisha Wawekezaji kuwekeza katika Sekta mbalimbali za kipaumbele nchini hususani Sekta ya Viwanda, Utalii, Nishati, uvuvi, usafirishaji ( Reli, Anga na Majini) na uchumi wa bluu.
Prof.Kahyarara ameyasema hayo Julai 5, 2022 alipokuwa akifungua Kongamano la Wawekezaji, Wauzaji na Wanunuaji lililofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam kama sehemu ya Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalianza tarehe 28 Juni hadi 13 Julai 2022
Akifungua kongamano hilo, Prof Kahyarara amewashauri wawekezaji wawekeze Tanzania kwa kuwa iko mahali pazuri kijiografia kwa kuwa na bahari inayowezesha usafirishaji wa mizigo, Raslimali za kutosha na Reli ya Kisasa inayoiunganisha na masoko ya ndani na nje ya nchi kupitia bandari.

Aidha, amesema Serikali imetenga maenwo mbalimbali ya uwekezaji ikiwa ni ni pamoja na uwepo wa kongani za viwanda zinazotarajiwa kuwa na viwanda vya kuchakata mazao na kuzalisha bidhaa mbalimbali pamoja maeneo maalumu ya uzalishaji bidhaa kwa ajili ya mauzo ya nje hususani karibu na viwanja vya ndege.
Aidha, Prof. Kahyarara aliwahakikishia wawekezaji kuwa Serikali inaendelea kuweka mazingira bora yanayovutia uwekezaji na ufanyaji biashara nchini kwa kurekebisha sera na sheria mbalimbali ikiwemo sheria ya uwekezaji, kuondoa baadhi ya tozo na kuanzisha Mfumo wa kielektroniki wa huduma za pamoja kwa wawekezaji.

Prof. Kahyarara pia ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutoa kipaumbele katika kukuza uchumi kwa kuchukua hatua mbalimbali za diplomasia ya uchumi ikiwemo filamu ya Royal Tour ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya kiuchumi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE Bi Latifa Mohammed Khamis amesema kupitia Kongamano hilo kuna baadhi ya Makubalino ya Kibiashara yatafikiwa ili kuhakikisha Fursa walizokuja nazo wawekezaji kupitia maonesho ya Saba saba zinawahufaisha watanzania nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news