Serikali yazindua Kikosi kazi cha Ulinzi kwa Watoto dhidi ya Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI Wa Katiba na Sheria, Mhe.Damas Ndumbaro amezindua kikosi kazi cha ulinzi kwa watoto dhidi ya biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu.
Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Damasi Ndumbaro akizungumza alipokuwa akizindua rasmi Kikosi kazi cha Ulinzi kwa watoto dhidi ya Biashara ya usafirishaji haramu wa Binadamu sambamba na kuzindua muongozo utakaowaongoza katika utendaji kazi wao. Hafla hiyo imefanyika Julai 21,2022 jijini Dar es Salaam.

Kikosi kazi hicho kimeanzishwa chini ya Mradi wa kupambana na Uhalifu mkubwa wa kupangwa ( Serious Organised Crime- SOC), ambacho kitatekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Akizindua kikosi kazi hicho, Waziri wa Katiba na Sheria, Julai 21, 2022 Dkt. Damas Ndumbaro, amesema athari ya uhalifu mkubwa wa kupangwa ni kubwa na inakuwa ya kushtukiza.
"Sisi, Tanzania tunayo mifano hai kuhusu madhara ya uhalifu wa aina hii, kwa mfano uripuaji wa mabomu katika ubalozi wa Marekani uliotekelezwa hapa kwetu, Kenya na Uganda kwa wakati mmoja,"amesema Dkt. Ndumbaro.

Amesema,kutokana na mikakati mbalimbali inayotekelezwa na Serikali katika mapambano dhidi ya ukatili na udhalilishaji wanawake na watoto, wameanza kushuhudia kuibuka kwa taarifa kuhusu uhalifu wa aina hiyo katika jamii na umeonesha bayana juu ya kazi kubwa iliyopo katika kukabiliana na janga hilo.

"Kwa maelezo hayo ninajenga hoja kwamba mradi huu wa kupambana na uhalifu mkubwa wa kupangwa hasa ule wa usafirishaji haramu wa Binadamu, unyonyaji na udhalilishaji wa watoto kingono ni muhimu sana na umekuja kwa wakati unaofaa katika nchi yetu," amesema Dkt Ndumbaro.
Kwa msingi huo, sisi sote tuliopewa dhamana ya kupambana na uhalifu mkubwa wa kupangwa kwa Makosa ya Biashara Haramu ya Binadamu, Ukatili na Udhalilishaji wa Watoto Kingono na Uhalifu Unaovuka Mipaka ya Nchi katika jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hatuna budi kuitumia fursa hii ili kuleta tija na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yetu ya kuhudumia taifa hili. Huu ni wakati wa kubuni mbinu mbali mbali zitakazoweza kubainisha hila na ghilba za wahalifu pia kubainisha changamoto zinazowakabili wapambanaji wa kazi hii na kutafuta mbinu muwafaka za kukabiliana nazo ili kufikia malengo tuliojiwekea.

Ubunifu wa mbinu mpya ni lazima utekelezwe sambamba na kuongeza uwezo wetu wa teknolojia ya mitandao ambayo baadhi ya wakati inatumika vibaya ili kuwanufaisha wahalifu wanaotaka mafanikio bila ya kufuata na kuheshimu sheria za ndani ya nchi na kimataifa.

"Kwa msingi huu sisi sote tuliopewa dhamana ya kupambana na uhalifu mkubwa wa kupangwa kwa Makosa ya Biashara Haramu ya Binadamu, Ukatili na Udhalilishaji wa Watoto Kingono na Uhalifu Unaovuka Mipaka ya Nchi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hatuna budi kuitumia fursa hii ili kuleta tija na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yetu ya kuhudumia taifa hili," amesema Dkt. Ndumbaro na kusisitiza.

"Huu ni wakati wa kubuni mbinu mbali mbali zitakazoweza kubainisha hila na ghilba za wahalifu pia kubainisha changamoto zinazowakabili wapambanaji wa kazi hii na kutafuta mbinu muwafaka za kukabiliana nazo ili kufikia malengo tuliojiwekea," amesisitiza.

Amesema, ubunifu wa mbinu mpya ni lazima utekelezwe sambamba na kuongeza uwezo wa teknolojia ya mitandao ambayo baadhi ya wakati inatumika vibaya ili kuwanufaisha wahalifu wanaotaka mafanikio bila ya kufuata na kuheshimu sheria za ndani ya nchi na kimataifa.
Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali, DPP Sylivester Mwakitalu akingumza alipokuwa akitoa salamu zake na hotuba fupi katika hafla hiyo.

Akizungumzumzia mradi huu, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) Slyvester Mwakitalu amesemea mradi huo ni wa miaka minne kuanzia Desemba, 2021 hadi Desemba 2025 na unatekelezwa kwa gharama ya dola za Kimarekani 6,434,320 ambapo zitatumika kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

"Mradi huu unatekelezwa kwa ufadhili wa Serikali ya Uingereza na Jumuiya ya Umoja wa Nchi za Ulaya kupitia Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) likishirikiana na, UNICEF na Shirika la Kimataifa la Uhamaji (IOM)" amesema Mwakitalu.

Mwakitalu amesema mradi huo umelenga kujenga uwezo wa kiutendaji kwa taasisi za Serikali zinazohusika katika utekelezaji wa sheria za kupambana na uhalifu mkubwa wa kupangwa ambapo kwa Tanzania Bara utajikita zaidi katika makosa ya biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu na udhalilishaji (unyanyasaji) wa watoto.

"Lengo kuu la mradi huu wa SOC ni kuvijengea uwezo vyombo vya ulinzi na usalama vinavyohusika katika utekelezaji wa sheria za mapambano dhidi ya uhalifu mkubwa wa kupangwa hasa katika nyanja za upelelezi, uendeshaji wa mashtaka na ulinzi kwa wahanga na manusura," Amesema Mwakitalu.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum, Dkt Dorothy Gwajima akizungumza kwenye hafla hiyo muda mfupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Dkt. ndumbaro kuzindua rasmi Kikosi kazi hicho.

Kwa upande wake, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto; Dk Doroth Gwajima amesema uzinduzi wa kikosi hicho umekuja wakati muafaka wakati Serikali ikiendelea kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news