SIKU YA KUZALIWA:Tufanye kazi kwa bidii asema Mheshimiwa Ndejembi

NA VERONICA SIMBA

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi ameadhimisha kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwake kwa kufanya kazi na kuhimiza wananchi na watumishi wa umma nchini kuitekeleza kwa vitendo kaulimbiu ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya KAZI IENDELEE. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akikata keki kuadhimisha kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwake. 

Mhe. Ndejembi amehimiza utekelezaji wa kaulimbiu hiyo kwa vitendo, akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Kijiji cha Naalarami wilayani Monduli. 

“Nimeadhimisha kumbukumbu ya siku yangu ya kuzaliwa kwa kufanya kazi siku nzima nikiwa katika ziara ya kikazi mkoani Arusha, na nawashukuru wananchi wa kijiji cha Naalarami kwa kunipatia zawadi ambayo itakuwa ni kumbukumbu kubwa maishani mwangu,” Mhe. Ndejembi amesema. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akiwashukuru walengwa wa TASAF wa Kijiji cha Naalarami Halmashauri ya Wilaya ya Monduli mara baada ya walengwa hao kumpongeza kwa kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, alipokuwa kwenye ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kwenye Kijiji hicho.

Ameongeza kuwa, katika kumbukumbu yake ya siku ya kuzaliwa ametumia fursa hiyo kuwaasa wananchi na watumishi wa umma kufanya kazi kwa bidii ili kuiishi kwa vitendo kaulimbiu ya Mhe. Rais ya KAZI IENDELEE. 

“Kwa watumishi wa umma mliopo hapa, hakikisheni mnachapa kazi kwelikweli usiku na mchana kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi hawa wa Kijiji cha Naalarami,” Mhe. Ndejembi amesisitiza. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akivalishwa vazi la Kimasai na walengwa wa TASAF wa Kijiji cha Naalarami Halmashauri ya Wilaya ya Monduli walipokuwa wakimpongeza kwa kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, alipokuwa kwenye ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika halmashauri hiyo.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amekagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba ya daktari inayojengwa kwa ufadhili wa OPEC (IV) kupitia uratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news