TANRADE yaingia makubaliano na Geita kuimarisha maonesho ya dhahabu

NA DIRAMAKINI

MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) imeingia makubaliano na Mkoa wa Geita kwa ajili ya kuimarisha maonesho ya dhahabu ambayo hufanyika kila ifikapo Septemba.
Akizungumza wakati wa utiaji saini wa makubaliano hayo uliyofanyika katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule amesema makubaliano hayo yatakwenda kuyafanya maonesho hayo ya dhahabu kuwa makubwa kuliko yote yanayofanyika hapa nchini.

Amesema, maonesho hayo ya dhahabu kuwa ya kitaifa yatasaidia kukua na kuwavutia wawekezaji wengi ndani na nje ya nchi kushiriki katika kuonesha bidhaa zao.

Senyamule amesema, Serikali imeridhia na kuyapandisha hadhi maonesho hayo ya dhahabu kuwa ya kitaifa hivyo makubaliamo hayo yatasaidia kuwa ya kisasa.

Amesema, baada ya makubaliano hayo TANTRADE pamoja Halmashauri ya Wilaya ya Geita watakaaa pamoja na kukubaliana namna bora ya kuyaboresha ili yaonekane ya hadhi na kisasa.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Geita, Zahara Michuzi amesema makubaliano hayo yatasaidia kuleta mapinduzi na kufanya mabadiliko kwenye teknolojia ya dhahabu.ndani ya mkoa wa Geita.

Amesema, wanataka kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya madini ya dhahabu hivyo kupanda hadhi kwa maonesho hayo kutachagiza mabadiliko hayo.

“Tumepokea kwa furaha nia njema ya kuingia makubaliano na TANTRADE kwani kutafanga maonesho hayo kutambulika nchini na kupanua wigo mpana wa ufanyaji biashara,”amesema. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TANTRADE, Latifa Khamis amesema kusainiwa kwa makubaliano hayo kutakwenda kuimarisha na kuufanya uwanja wa Geita kuwa wa kisasa kwa ajili ya maonesho hayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news