Tanzania, Iran kuendelea kudumisha misingi ya kibiashara

NA DIRAMAKINI

MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) imesema, uhusiano wa nchi ya Tanzania na Iran utasaidia kudumisha misingi ya kibiashara katika majukumu ya pamoja na kuhakikisha kila mmoja anatumia fursa za mwezake katika kuendeleza kibiashara.
Mkurungezi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE ), Latifa Khamis akimueleza jambo Kaimu Balozi wa Iran, Hussein Bahineh leo katika Maadhimisho ya Siku ya Iran ambayo yamefanyika katika maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 46 yanayoendelea viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Saaalm.

Hayo yamebainishwa leo Julai Mosi na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Latifa Khamis wakati wa maadhimisho ya Siku ya Iran yaliyofanyika katika viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba).

Amesema, ni wakati sasa watanzania kuweza kutumia fursa mbalimbali za kibiashara zinazojitokeza katika nchi ya Iran. 

Amesema, lengo la kuja na siku hiyo ambayo ni ya kwanza katika maonesho hayo ya 46 yanayoendelea, "ni kuadhimisha mahusiano ya Tanzania na Iran ambayo ni ya miaka 40 sasa katika maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 46 kwa sababu tunatilia mkazo fursa baina ya nchi hizi mbili".

"Tumeona tusitumie maonesho haya kwa kutembelea na kuona tu, bali kuudumisha kwa misingi ya kibiashara katika majukumu yetu yanayotukabili kila siku kuhakikisha nchi zetu kila mmoja inatumia fursa ya mwenzie katika kuendelea biashara,"amesema.

Aidha, aliwataka watanzania kuweza kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza katika nchi ya Iran ili kuamsha zile fursa ambazo hatujazitumia.

Aliongeza kuwa, ziara ya Iran imelenga kuonesha fursa zilizopo kwao ambazo kwa nchi yetu tunaweza kuzitumia katika maeneo mbalimbali. 

Kwa upande wake Kaimu Balozi wa Iran, Hussein Bahineh alisema nchi ya Iran imejikita katika uwekezaji hasa sekta ya gesi, madini, teknolojia.

"Tunafurahi kuwepo katika maonesho haya kusherehekea ushirikiano wetu uliodumu muda wa miaka 40, na tutaendelea kushirikiana na Tanzania katika mambo mbalimbali, "amesema Bahineh.

Post a Comment

0 Comments