Waziri Dkt.Tax avutiwa na miradi ya SUMAJKT, atoa wito

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt.Stergomena Tax amesema Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) ni mahali sahihi pa biashara na uwekezaji kutokana na kufanya shughuli mbalimbali ambazo zimekuwa zikichangia katika uchumi wa nchi.
Dkt.Tax ameyasema hayo jijini Dar es salaam leo katika maadhimisho ya miaka 41 ya SUMAJKT ambayo yamefanyika katika Maonesho ya Biashara ya kimataifa 46 yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere.

Amesema, SUMAJKT imekuwa ikifanya Shughuli mbalimbali za kuendeleza uchumi wa nchi katika maeneo mbalimbali ya kiuchumi na kijamii.

Akitaja baadhi ya Shughuli hizo ni pamoja na viwanda ambayo vimekuwa vikichangia kwa kiasi kikubwa katika sekta ya kilimo, viwanda vinavyozalisha na kufanya uchakataji wa bidhaa mbalimbali, viwanda vya ujenzi , viwanda vya kutengeneza bidhaa za majumbani pamoja na viwanda vya kutoa Huduma muhimu Kama afya, huduma kibandari.

"Jukumu kubwa la Jeshi ni kulinda mipaka ya nchi na uhuru wake hivyo uhuru ni lazima ujitengemee kiuchumi hivyo SUMAJKT imekuwa ikifanya kazi ya kuchangia na kujitegemea kiuchumi na kijamii na kubaki imara kama taifa,"amesema Dkt.Tax.
Aliongeza kuwa, shughuli hizo za SUMAJKT zimekuwa zikitekelezwa na vijana wa JKT hususani vijana wa kujitolea .

"Katika Shughuli hizi mlizoziona vijana hawa wanapata stadi mbalimbali wanapotoka pale nao wanakwenda kujitegemea "amesema

Aidha alitoa wito kwa vijana wote ambapo wamekuwa wakipata stadi hizo baada ya kizipata wazitumie ipasavyo kwa kuweza kuanzisha Shughuli zao za kiuchumi na hatimaye wajitegemee na kuwafundisha wengine.

Vilevile Dkt.Tax amesema, SUMAJKT pia imejipanga ambapo katika bajeti ya mwaka huu kunaongezeko la miradi ya maendeleo ya zaidi ya asilimia 260.
"Ongezeko hili haliwezi kukidhi miradi yote kikubwa katika ongezeko hili ni miundombinu kwa ajili ya miradi ya kimkakati ya kilimo ambacho ni kitu kikubwa sana pamoja na kuweka sawa miundombinu kwa ajili ya vijana,"amesema. 

Na kuongeza kuwa, "Katika bajeti ya Serikali ya mwaka huu msisitizo mkubwa umekuwa katika sekta ya uzalishaji hivyo pia sisi tutafanya kazi na wadau mbalimbali,"alisisitiza.

Katika hatua nyingine Dkt.Tax alitoa wito kwa SUMAJKT licha ya kufanta Mambo mengi katika miaka 41 aliwataka kuangalia eneo moja na kuhakikisha wanajipanua na kuwez kufika sehemu mbalimbali.

"Hii miradi ya vikosi itaendelea kuwepo lakini ni muhimu kuwa miradi mikubwa ya kitaifa ambayo ndiyo maono tuliyonayo katika kusherehekea miaka 41,"amesema Dkt.Tax.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news