TARURA yatakiwa kuweka nguvu katika ujenzi wa barabara za mawe

NA THERESIA MWAMI

BODI ya Mfuko wa Barabara nchini imeitaka Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA), kuweka nguvu katika ujenzi wa barabara za mawe kwa kuwa zinadumu na gharama za ujenzi wake ni nafuu.
Kijana pichani (jina halikupatikana) akichonga mawe katika machimbo ya Nyashada, kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya mawe ya Nyanda (m370) iliyoko Igoma jijini Mwanza, wakati wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB) wakikagua machimbo hayo.

Hayo yalielezwa jana na Makamu Mwenyekiti wa bodi hiyo, Octavian Mshiu alipokagua barabara ya shule ya msingi Igoma yenye urefu wa mita 370 na Nyashana mkoani Mwanza ambazo zote zimejengwa kwa mawe.
Mwanamama pichani (jina halikupatikana), akikusanya mawe aliyoyachonga katika machimbo ya Nyashada, kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya mawe ya Nyanda (m370), iliyoko Igoma jijini Mwanza, wakati wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB) wakikagua machimbo hayo. (Picha na Theresia Mwami).

Alisema sio Mwanza pekee, bali mkoa wowote wenye uwezo wa kujenga barabara kwa kutumia teknolojia mbadala ikiwemo mawe, unapaswa kufanya hivyo ili kuepuka gharama na kuzuingatia uimara.

"Tutajenga barabara nyingi zaidi za mawe kuliko kutegemea lami ambayo tunaagiza nje ya nchi," alisema.
Paulo Malima ambaye ni Msimamizi Mkuu wa Uzalishaji kutoka kampuni ya inayojenga barabara ya mawe ya Ndama (mita 370) iliyopo Igoma jijini Mwanza, akifafanua jambo kwa wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB), wakati wakikagua barabara hiyo.

Meneja wa Tarura wa mkoa huo, Mhandisi Gudluck Mbanga alisema pamoja na uimara wa barabara za mawe, pia ujenzi wake unatengeneza fursa za ajira kwa makundi mbalimbali ya wananchi.

"Kwa kifupi inatusaidia sana kwa sababu Jiji la Mwanza lina miinuko yenye mawe ambapo barabara za gravu zinashindwa kupitika hasa wakati wa mvua," alifafanua.
Muonekano wa barabara ya Ndama (mita370), iliyopo Igoma jijini Mwanza inayojengwa kwa kiwango cha mawe, kwa gharama ya shilingi za kitanzania milioni 167.1. Ujenzi wa Barabara hiyo unasimamiwa na Ofisi ya Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Nyamagana.

Katika Jiji hilo, alibainisha kuna jumla ya kilomita 2,000 za mtandao wa barabara zinazo simamiwa na TARURA, ambapo kati ya hizo mtandao wa barabara za mawe ni kilomita 16 pekee sawa na asilimia 0.2.

Naye Mhandisi wa barabara wilayani Nyamagana, Jane Mdula alisema kwa sehemu kubwa ujenzi wa barabara za mawe unafanywa na watu na sio mitambo.

Alitolea mfano gharama za ujenzi wa barabara ya Igoma yenye urefi wa mita 370 ambayo ujenzi wake unagharimu Sh167 milioni na kwamba imezalisha ajira lukuki za uchongaji mawe kwa wananchi wa kawaida.

Matumizi ya mawe katika ujenzi wa barabara, yameleta fursa ya kipato kwa wafanyakazi katika mgodi wa mawe, alisema Irene Musa mkazi wa Mkoa huo.

Hata hivyo Ibrahim Musa, kijana mwenye umri wa miaka 18 anayefanya kazi kwenye machimbo hayo, ameeleza kuwa kupitia shughuli ya uchongaji wa mawe yanayotumika katika ujenzi wa barabara ameweza kujiingizia kipato ambacho hukitumia kuwasaidia wazazi wake.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara Octavian Mshiu akimuelekeza jambo Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Goodluck Mbanga (wa kwanza kulia), wakati wajumbe wa Bodi hiyo wakikagua machimbo ya mawe ya kujengea barabara yaliyoko Nyashada jijini Mwanza.

Ujenzi wa barabara za mawe unatajwa kuwa ni wagharama nafuu ukilinganisha na ule wa barabara za lami, lakini pia unatoa fursa nyingi za ajira kwa wananchi wenye uwezo wa kushiriki kwenye kazi za ujenzi wa barabara, vilevile unasaidia kufungua barabara na kuwawezesha wananchi kufikia huduma za kijamii kama shule na hospitali kwa urahisi zaidi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news