VETA kuanzisha mfumo wa mafunzo ya vitendo katika teknolojia ya viwanda

NA DIRAMAKINI

MWENYEKITI wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA),Dkt. Peter Maduki amesema, wamejipanga kuanzisha mfumo wa mafunzo ya vitendo ambao utakwenda sambasamba na teknolojia ya viwanda.
Maduki ameyasema hayo wakati akikagua bunifu mbalimbali katika Banda la VETA ndani ya Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu Sabasaba.

Amesema, mafunzo hayo yatawasaidia wanafunzi kuweza kujiajiri wenyewe na si kusubiri kuajiriwa.

"Lengo letu ni kutaka kufikia vijana 700,000 ndani ya miaka mitano wapitie katika vyuo vyetu na kujipatia ujuzi wa aina mbalimbali,"amesema Dkt.Maduki.

Amesema, vijana hao watapitia mfumo wa mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi na kupatiwa vyeti vyao.

"Na katika hao 700,000 hatutegemei waajiriwe bali wengine wajiajiri na kuzalisha ajira pia waweze kusaidia wawekezaji watakaokuja nchini,"amesema Dkt.Maduki.

Aidha, amesema VETA wamekuwa wakiwasaidia wale wanaofanya vizuri kwa kiwaungajisha na Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) ili waweze kuendelezwa.

"Kwa mwaka jana peke yake tuliweza kusaidia wabunifu watano kuendelezwa na Costech,"amesema.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Veta Tanzania, Antony Kasore amesema wanazalisha nguvu kazi kulingana na sekta za kimkakati.

"Tunafundisha vijana namna ua kufanya kazi migodini, katika gesi ili wawezenkuwa msaada,"amesema Kasore.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news