Kamishna wa TIRA atembelea banda la NIC, asisitiza jambo

NA DIRAMAKINI

KAMISHINA wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima Nchini (TIRA), Dkt.Baghayo Saqware amesema, Serikali ipo tayari kushirikiana na Shirika la Bima la Taifa (NIC) kwa kuhakikisha inawafikia wakulima, wafugaji, na wavuvi wote nchini.
Dkt.Saqware ameyasema hayo alipotembelea katika banda la NIC lililopo katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa 46 yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Amesema, Serikali imekuwa ikitegemea sana Shirika la NIC katika kuendeleza soko katika maeneo ya bima ya kilimo, majengo, pamoja na bima mbalimbali.

Dkt.Sqware amesema, NIC ni wazoefu zaidi katika soko la bima kutokana kwani wamekuwa na mtaji mkubwa na wataalamu wa kutosha katika soko.

"Ukizungumzia bima Tanzania hakuna namna unaweza kuisahau NIC kwa maana ya wataalamu, uzoefu pamoja na mtaji,"amesema Dkt.Sqware.

Vilevile amesema hivi karibuni NIC wamejikita katika bima ya kilimo ambapo amewapongeza kwa hatua hiyo na kuhaidi kuendelea kushirikiana nao.

"Tayari tumewapatia namba viongozi wa NIC ili waweze kuwasiliana na viongozi wa wakulima na wafugaji hapa nchini ili waaze kuangalia ni kwa namna gani wanaweza kuwafikia zaidi na kuwapatia bima,"amesema.

Naye Mkurungezi wa Masoko na Huduma kwa Wateja NIC, Yesaya Mwakifulele amesema katika Maonesho hayo NIC imejikita katika ushiriki kikamilifu kwa kuhakikisha inatoa huduma mbalimbali kuhusu suala nzima la bima.

Amesema katika maonesho hayo wamekuja na APP ya NIC kigajani ambayo inamuwezesha mteja kupata huduma akiwa nyumbani bila ya kufika katika ofisi zao.

"Kupitia APP hiyo mteja anaweza kujihudumia kwa hatua chache tu ambayo ataweza kukata bima ya aina mbalimbali ikiwemo nyumba, gari,"amesema.

Akizungumzia kuhusu suala nzima la madai amesema, NIC imekuwa ikifanya ulipaji huo ndani ya siku saba tu iwapo taarifa zote zikiwa sawa.

"Kwa sasa hatuna madai yoyote ambayo hayajalipwa labda yale ambayo taarifa zake haziko sawa,"amesema Mwakifulele.

Aidha, amewataka watanzania wote kwa ujumla kufika atika banda lao ili waweze kupata elimu pamoja na huduma za uhakika za bima ambazo zitaweza kumsaidia pale anapopata majanga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news