Wafugaji watakiwa kuchanja mifugo yao kuyakabili mapele ya ngozi

NA DIRAMAKINI

SERIKALI wilayani Nkasi mkoani Rukwa imewataka wafugaji kuichanja mifugo yao ili kuweza kukabiliana na ugonjwa wa mapele ya ngozi. 
Ugonjwa wa mapele ya ngozi ni moja kati ya magonjwa yanayoitesa mifugo hasa ng’ombe na kupelekea kifo, lakini pia hata ngozi kuharibika na kuharibu bidhaa ya ngozi na kuathiri uchumi kwa mfugaji ikiwa ni pamoja na taifa kwa ujumla.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa chanjo ya pili ya ugonjwa huo kwa mifugo Katibu tawala wa wilaya, Cosmas Kuyela alisema kuwa ni lazima kwa wafugaji wote kuhakikisha wanaichanja mifugo yao kwani itakuwa haina maana kama wachache watachanja mifugo yao na wengine wakabaki. 

Alisema kuwa, ugonjwa huo unaambukiza hivyo kama tumeamua kuingia kwenye mapambano ya kukabiliana na ugonjwa huo ni lazima mifugo yote ichanjwe na kuwa uzuri kuna sheria inayowataka wafugaji kutekeleza jukumu la kuichanja mifugo yote. 

Afisa mifugo wa wilaya, Dkt.John Shauri Tlatlaa alisema kuwa ili kuweza kukabiliana kabisa na ugonjwa huo ni lazima chanjo hiyo ifanyike kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo nah ii ni chanjo ya pili na kuwa mwakani wataikamilisha chanjo yas tatu. 

Alisema kuwa, kwa mujibu wa sheria ya mifugo ya mwaka 2020 inasema kuwa yeyote ambaye hatachanja mifugo yake atalipa faini ya shilingi Mil,2 au kwenda jela mwaka mmoja au vyote kwa pamoja. 

Diwani wa Kata ya Chala, Michael Mwanalinze kwa upande wake aliwasihi wafugaji kutekeleza jukumu hilo la kuhakikisha mifugo yao yote inachanjwa kwani hilo ni faida kubwa sana kwao kwa maana mifugo itakua salama. 

Pia aliwataka kutofanya ujanja wa kukwepa kuichanja mifugo yao kwa maana sheria ipo ni vyema wakatii sheria bila shuruti badala ya kusubiri sheria kuchukua mkondo wake pale itakapobainika kuwa wamevunja sheria kwa kutoichanja mifugo yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news