Watakiwa kujiunga na Chama cha Wajane Tanzania (CCWWT)

NA DIRAMAKINI

WANAWAKE wajane mkoani Rukwa wametakiwa kujiunga na Chama cha Wajane Tanzania (CCWWT) kuweza kukusanya nguvu itakayowawezesha kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili. 
Wito huo umetolewa jana na mratibu wa chama hicho ngazi ya Taifa, Sabrina Tenganamba alipozungumza na Wanawake Wajane katika lengo la kufanya uchaguzi wa kupata viongozi wa chama hicho ngazi ya mkoa na wilaya. 

Alisema kuwa, uundwaji wa chama hicho umelenga kuwaunganisha wanawake wote wajane nchini ili kurahisisha kushughulikia changamoto zinazowakabili Wanawake wajane hasa zile za kisheria.

“’Wanawake wajane wengi wetu wanakabiliwa na changamoto kubwa katika familia zao ikiwemo ya kunyang’anywa mali na kunyanyapaliwa hivyo chama hiki kitakuwa na jukumu hilo la kuangalia chamgamoto hizo na kuzikabili,”alisema. 

Mratibu huyo wa CCWWT taifa alidai kuwa, wajane wengi wamekuwa wakifariki kutokana na changamoto mbalimbali hasa ya msongo wa mawazo baada ya kupitia manyanyaso mengi na kuishi maisha magumu ukilinganisha na alipokuwa akiishi na mmewe kabla ya kufariki. 

Pia alifafanua kuwa chama hicho kitakuwa na jukumu la kuwajengea uwezo Wanachama wake katika kuona wanapata elimu ya ujasiriamali na kuendesha shughuli za kujikimu kimaisha ikiwa ni pamoja na kuona kuwa wananufaika na mikopo mbalimbali hasa ile inayotolewa na serikali. 

Mlezi wa chama hicho mkoani Rukwa, Anastela Maraji (Mama John) alidai kuwa, wajane wamepata ukombozi na kumtaka kila mmoja kuhakikisha anajiunga ili aweze kunufaika na fursa zitakazopatika kubwa ni la mikopo isiyo na riba ili kuweza kushughulika na shughuli za kiuchumi ikiwa ni pamoja msaada wa kisheria. 

Katika mkutano huo waliweza kuchaguana na kupata viongozi ambapo katika ngazi ya mkoa mwenyekiti ni Mariamu Megiji na Aurelia Kanyengele katibu. 

Ngazi ya wilaya waliochaguliwa Wilaya ya Nkasi Crista Credo Sangu ni mwenyekiti na Suzana Milambo ni katibu na wilaya ya Sumbawanga waliochaguliwa ni Femiotha Daniel Mwenyekiti na Janeth Kakisanya ni katibu. 

Wilaya nyingine ambazo hazipata viongozi zimepewa muda ili zikamilishe mchakato huo ikiwa ni pamoja na kupata viongozi ngazi ya kata.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news