Wananchi wamiminika Banda la Benki Kuu Tanzania (BoT) katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba)

Kaimu Meneja, Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki BoT, Bi. Victoria Msina, akitoa maelezo kwa Naibu Gavana, Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Bi. Sauda Kassim Msemo (kulia) alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja Idara ya Majanga BoT, Bi. Dorosela Blasius na Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki BoT, Bw. Augustino Hotay. 
Naibu Gavana, Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Bi. Sauda Kassim Msemo, akiweka saini katika kitabu cha wageni alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam. 
Naibu Gavana, Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Bi. Sauda Kassim Msemo, akifurahia jambo na Afisa Rasilimali Watu Mwandamizi kutoka Bodi ya Bima ya Amana, Bi. Joyce Shala na Afisa wa Benki Bi. Rukia Muhaji katika banda la Benki Kuu ya Tanzania kwenye Maonesho ya Sabasaba. Mhasibu Mkuu Mwandamizi BoT, Bw. Elirehema Msemembo, akielezea sarafu za BoT kwa watoto waliotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam. 
Afisa Mkuu Mwandamizi wa Uhusiano wa Umma BoT, Bw. Lwaga Mwambande, akielezea namna ya kutambua Alama za Usalama za noti zetu kwa wananchi waliotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam. 
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Shilole akitazama picha za noti za Benki Kuu ya Tanzania alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Afisa Uhusiano wa Umma na Itifaki, Bi. Beatrice Ollotu. Mchambuzi wa Masuala ya Kifedha BoT, Bi. Laila Kisombe akitoa elimu kuhusu Uwekezaji katika Dhamana za Serikali kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki BoT, Bw. Augustino Hotay akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa Utumishi na Uendeshaji BoT, Bw. Kened Nyoni, walipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam.(Picha zote na BoT).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news