WAZIRI BALOZI DKT.CHANA ATEUA WAJUMBE SABA WA BODI YA MAMLAKA YA HIFADHI YA ENEO LA NGORONGORO (NCAA)

NA DIRAMAKINI

 

KUFUATIA Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumteua Jenerali (Mst) Venance Salvatory Mabeyo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) tarehe 30 Juni, 2022, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi H. Chana (Mb) kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 5(2) cha Sheria ya Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Sura ya 284 kikisomwa pamoja na Jedwali la Pili, Kipengele Na. 1 na 2(1)(b)-(c), amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Bodi ya NCAA:-

 

  1. Bw. Benson Obdiel Kibonde, Mhifadhi Wanyamapori Mkuu (Mst) Pori la Akiba Selous.
  2. Bw. Bakari Nampenya Kalembo - Mshauri wa Masuala ya Fedha.         
  3. Bibi Agnes Kisaka Meena, Mkurugenzi wa Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.                                
  4. Prof. Esther William Dungumaro, Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu, Mkwawa (MUCE).                        
  5. Prof. Herrieth Godwin Mtae, Mtaalamu wa Maendeleo ya Uchumi wa Jamii, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).                         
  6. Prof. Henry Chalu, Profesa Mshiriki, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.                 
  7. Bw. Simon Vedastus Ntobbi, Afisa Tawala Mkuu Daraja la I, Ofisi ya Rais - UTUMISHI.

            

Uteuzi huu ni wa miaka mitatu kuanzia tarehe 20 Julai, 2022 hadi 19 Julai, 2025.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news