Rais Samia aunda Kamati na Sekretarieti zitakazoshauri namna ya kuleta mabadiliko ya utendaji kazi wenye matokeo bora

NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameunda Kamati na Sekretarieti zitakazoshauri namna ya kuleta mabadiliko ya utendaji kazi wenye matokeo bora katika vyombo vya utendaji haki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali katika Hafla ya kumwapisha Mkuu mpya wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Camillus Mwongoso Wambura na baadhi ya Mabalozi aliowateua kwenye Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.

Rais Samia amesema hayo katika hafla ya uapisho wa Viongozi mbalimbali iliyofanyika Ikulu Chamwino, akieleza kuwa Kamati hiyo itaongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu, Mhe. Mohamed Chande Othman.

Aidha, Rais Samia amesema Kamati hiyo itaanza kulifanyia kazi Jeshi la Polisi na baadae katika majeshi mengine ya ulinzi na vyombo vya utendaji haki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Rais Samia pia amesema Serikali itapitia na kurekebisha miundo, mifumo ya ajira na mafunzo, mifumo ya upandishaji vyeo, madaraka na taaluma za kijeshi.

Masuala mengine ni kutoa mafunzo kwa majeshi ya ulinzi kuhusu matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano pamoja na mahusiano ya Jeshi la Polisi na Taasisi zingine ikiwemo Kanuni na Sheria zinazoongoza Taasisi hizo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na CP Mussa Ali Mussa kushoto, Kamishna wa Fedha na Lojistik CP Liberati Sabas Materu, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Makao Makuu ya Polisi CP Awadhi Juma Haji, na Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad katika Hafla ya kumwapisha (IGP) Camillus Mwongoso Wambura Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.

Kwa upande mwingine, Rais Samia amelitaka Jeshi la Polisi kufanya kazi kwa ufanisi, na kuimarisha usalama wa raia na mali zao na kuzingatia haki za binadamu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news