Waziri Bashungwa amtembelea Sheikh wa Mkoa wa Kagera, wateta

NA OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Innocent Bashungwa amewasili mkoani Kagera leo Julai 12, 2022 na kupata fursa ya kufanya mazungumzo na Sheikh wa Mkoa wa Kagera, Alhaji Haroun Abdallah Kichwabuta.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofisi zake zilizopo katika Masjidil Munawwaru maarufu kama Msikiti wa Bilele Manispaa ya Bukoba, Kagera.
Katika Mazungumzo hayo Sheikh Haroun amemuelezea Waziri Bashungwa juu ya Mpango wa Miaka Mitano ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) mkoani Kagera ambao ni pamoja na ujenzi wa vituo vya afya katika kila wilaya zinazounda mkoa huo.
Waziri Bashungwa amewashukuru viongozi wa taasisi za kidini kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kuwahudumia wananchi kupitia sekta mbalimbali kama afya, elimu na maji na akawahakikishia ushirikino wa kutosha kati ya Serikali na taasisi hizo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news