Waziri Mkenda ampokea Waziri Ofisi ya Rais wa Sudan Kusini, Dkt.Benjamin

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Elimu, Sayansi, na Teknolojia, Mhe. Prof Adolf Mkenda (Mb) leo Julai 20, 2022 amempokea Waziri Ofisi ya Rais wa Sudan Kusini. Mhe. Dkt Barnaba Marial Benjamin katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Dkt.Barnaba amewasili nchini kwa ajili ya kumwakilisha Rais wa Sudan Kusini, Mhe. Salva Kiir kwenye Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika kuanzia tarehe 21-22 Julai 2022 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano-AICC jijini Arusha.

Post a Comment

0 Comments