Waziri Ummy aipongeza TMDA kwa kuwa mstari wa mbele kutoa elimu

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu ameipongeza Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba(TMDA) kwa namna inavyotoa elimu kuhusiana na masuala mbalimbali katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba mkoani Dar es Salaam. 
Pongezi hizo amezitoa alipotembelea katika banda hilo ambapo amefurahiswa na mamlaka hiyo kushiriki katika maonesho hayo.

TMDA imekuwa ikitoa elimu kwa wananchi kuhusu ubora, usalama na ufanisi wa bidhaa za dawa,vifaa tiba pamoja na vitendanishi.

Pia aliipongeza TMDA kwa kutoa elimu kuhusiana na madhara yanayotokana na matumizi ya bidhaa za tumbaku.

Kingine ambacho Waziri Ummy Mwalimu amefurahiswa ni kuona TMDA inajipanga katika kuhakikisha masuala mazima ya kutoa elimu hususani katika kueleza kemikali ambazo zipo katika bidhaa za tumbaku na katika kuelezea wamekuwa wakionesha kemikali za sumu ambazo zinapatikana kwenye tumbaku.

Hivyo amefurahi kuona wananchi wanapata uelewa kwa sababu suala zima la matumizi ya tumbaku linahitaji mtu awe na uelewa anapoingia katika matumizi yale ajue kabisa nini matokeo yake.

Akiwa katika banda hilo, maofisa wa TMDA wakiongozwa na Mkurugenzi wao Adam Fimbo walimueleza Waziri kuwa wamekuwa wanahusisha wadau ambao wanamiliki maeneo ya wazi kuzingatia yale yanayotakiwa kufanyika kwa maana ya kutenga eneo maalum ya uvutaji lakini waweke alama za kuonesha No Smoking na Smoking area.

Lengo la kufanya hivyo ni kumkinga asiyetumia na wanaotumia wajue nini kitatokea kutokana na matumizi ya tumbaku.

Waziri Ummy ambaye alikuwa ameambatana na Mratibu wa Kimataifa wa Mapambano ya UVIKO-19 kutoka Umoja wa Mataifa, Dkt.Ted Chaiban ambapo naye ameonesha kufurahia hatua zinazochukuliwa na TMDA katika kuelimisha umma kuhusu usalama na ubora wa dawa na vifaa tiba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news