Askofu Dkt.Brown Mwakipesile ahimiza waumini kushiriki Sensa Agosti 23 kikamilifu

NA MWANDISHI WETU

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la E.A.G.T nchini Dkt. Brown Abel Mwakipesile amewaasa washirika wa kanisa hilo kushiriki kikamilifu katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi linalotarajiwa kufanyika Agosti 23, 2022 kwa kuzingatia umuhimu wa zoezi hilo katika maendeleo ya nchi yetu.
Askofu Mwakipele ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuhitimisha ibada maalum ya kumaliza mkutano mkubwa wa injili wa kanisa hilo tarehe 7 Agosti, 2022 katika kanisa lake lililopo Maili Mbili jijini Dodoma.
Mwimbaji wa nyimbo za Injili Sifael Mwabuka akihudumu wakati wa ibada hiyo.
Alisema, kila muumini anawajibika kushiriki katika Sensa ya Watu na Makazi kwa kuzingatia umuhimu wake, katika mipago mbalimbali ya maendeleao ya nchi.
Askofu Mkuu wa Kanisa la E.A.G.T nchini Dkt. Brown Abel Mwakipesile akihuiri wakati wa ibada ya kuhitimisha mkutano wa injili wa Kanisa la E.A.G.T Mlimwa West Jijini Dodoma tarehe 7 Agosti, 2022.

“Kila mmoja aone umuhimu wa kushiriki katika zoezi hili, ili kusaidia Serikali yetu katika kurahisisha mipango ya maendeleo iliyopo kufanikiwa,”alisema Dkt. Mwakipesile
Mwimbaji wa nyimbo za injili Jonson Sifael akiimba wimbo wakati wa ibada hiyo.

Aliongezea kuwa, wataendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa maendeleo anayoyafanya katika nyanja mbalimbali ikiwepo kuitangaza nchi kimataifa.
Baadhi ya waimbaji wa kwaya ya New Jerusalem wakimsifu Mungu wakati wa ibada hiyo.
Baadhi ya washirika wakiomba wakati wa ibada hiyo.
Mwinjilisti Anthony Wambura akiwaombea watu waliookoka kwenye mkutano wa injili wa kanisa la EAGT Mlimwa West mara baada ya kuhubiri ibada maalum ya kuwakaribisha kanisani hapo.

Aidha,Askofu Dkt. Mwakipesile ametoa shukrani pamoja na pongezi kwa serikalii kwa namna inavyotoa nafasi na vibali katika kuhubiri injili ambayo ndiyo lengo la kanisa hilo ili kila mtu afikiwe na injili na kuacha dhambi na kutenda mambo mema.
Mwimbaji wa nyimbo za injili Easther Sifael akiimba wimbo wakati wa ibada hiyo.

''Naishukuru sana Nchi yetu kwa vile ambavyo imetoa uhuru wa kwamba neno la Mungu lihubiriwe kwa watu wote katika Nchi yetu kwa sababu neno la Mungu ndio Baraka na Ufunguo pekee katika Maisha ya Mwanadamu,' alisisitiza Askofu Mwakipesile.

Hata hivyo, Askofu Mwakipesile amebainisha kuwa katika mkutano uliokuwa ukifanyika kanisani hapo kwa muda wa siku nane umekuwa wa baraka na miujiza mkubwa imetendeka ikiwemo watu kufunguliwa katika mateso mbalimnbali ikiwemo magonjwa na watu wengi kufunguliwa vifungo vilivyokuwa vinatesa maisha yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news