BADO SIKU 7:HIZI HAPA TAARIFA MUHIMU SIKU YA SENSA

NA DIRAMAKINI

SENSA itafanyika usiku wa tarehe 22 Agosti, 2022 kuamkia tarehe 23 Agosti, 2022. Siku ya Sensa tarehe 23/8/2022 itabaki kuwa tarehe rejea ya Siku ya Sensa.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), zoezi la Kuhesabu Watu litaendelea kwa takribani siku sita na ieleweke kuwa Sensa haiwezi kukamilika kwa siku moja kwa nchi nzima.
Hivyo, wananchi wote watapaswa kuendelea na majukumu yao ya kila siku lakini Wakuu wa Kaya wanapaswa kuhakikisha kuwa WATU WOTE WALIOLALA KWENYE KAYA USIKU WA TAREHE 22 Agosti, 2022 KUAMKIA TAREHE 23 AGOSTI, 2022 wanaorodhesha taarifa zao muhimu ikiwemo:-

1. Jina kamili (majina matatu)

2. Jinsia (me/ke)

3. Umri

4.Hali ya ndoa

5. Namba ya simu

6. Namba ya Nida

7. Taarifa za Elimu

8. Taarifa za hali ya afya

9. Umiliki wa Ardhi, Majengo, vifaa/rasilimali

10. Taarifa ya Shughuli za Kiuchumi

11. Mengineyo (uraia)

Pamoja na kuacha taarifa hizo Karani wa Sensa atakapofika kwenye Kaya yako atakupigia simu kuhakiki taarifa ulizoacha. Sensa kwa Maendeleo, Jiandae Kuhesabiwa tarehe 23 Agosti, 2022.

Post a Comment

0 Comments