Diploma waliopungukiwa GPA kidogo waitwa kujiunga Foundation Program ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania

NA DIRAMAKINI

KAMA wewe una Diploma na GPA yako ni 2.9-2.0 basi sifa zimepunguwa kidogo na hivyo huwezi kujiunga na Shahada ya Kwanza. Njoo Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ujiunge foundation ili uweze kupata sifa za kujiunga na Shahada mara utakapohitimu foundation.
Kumbuka, ili uweze kujiunga foundation, wewe mwenye Diploma unapaswa kuwa na Award Verification Number (ANV) inayotolewa na NACTVET. Ikiwa huna AVN huwezi kuchaguliwa kwani sifa zitakuwa hazijatimia.

Pia, tunawakumbusha, kwamba foundation programu inachukuwa wenye form Six waliopungukiwa sifa kidogo kama ilivyoelezwa kwenye matangazo yetu mengine. Masomo yataanza mwezi Novemba 2022 mpaka Juni 2023. Tuma maombi yako sasa hivi kupitia www.out.ac.tz BURE.

Kama una swali usisite kuandika ujumbe kupitia nambari 0719017254. Au fika tawi la karibu la Chuo Kikuu Huria cha Tanzania utahudumiwa.

WENU

Dkt.Mohamed Omary Maguo
Mhadhiri na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania

Post a Comment

0 Comments