BREAKING NEWS: Rais Samia amteua Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza usiku huu

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amemteua SACP Mzee Ramadhan Nyamka, Kaimu Kamishna wa Magereza Huduma za Urekebu kuwa Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 26, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi.Zuhura Yunus.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,uteuzi wa SACP Mzee Ramadhan Nyamka umeanza Agosti 24, 2022.

Aidha, SACP Ramadhan anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee ambaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Post a Comment

0 Comments