CAF African Super League kuzijaza mabilioni ya fedha klabu Afrika

NA DIRAMAKINI

SHIRIKISHO la Soka barani Afrika (CAF) leo Agosti 10, 2022 limezindua mashindano mapya yatakayovishirikisha vilabu 24.

Mashindano hayo ya CAF African Super League yanalenga kuleta mapinduzi ya soka barani Afrika na yanakuwa mashindano yenye thamani kubwa zaidi.

Hayo yametangazwa na Rais wa CAF, Patrice Motsepe saa chache tu baada ya shirikisho hilo kuripoti hasara ya zaidi ya dola milioni 50 kwa mwaka jana.

Rais Motsepe amesema katika mkutano mkuu wa CAF uliofanyika Arusha, nchini Tanzania kuwa, ligi hiyo mpya itatoa zawadi ya kifedha ya jumla ya dola milioni 100 ikiwa ni mara tano zaidi ya kiasi kinachotolewa kwa sasa katika Ligi ya Mabingwa ya CAF.

Hata hivyo, Rais huyo hakuweka wazi ni vilabu gani 24 vya Afrika vitakavyoshiriki katika msimu wa kwanza, wala kutoa maelezo ya muundo halisi wa mashindano hayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

  1. Lkn kwa Tanzania TFF ina siasa chafu chafu na ubabe wa Kiushabiki, wa kuibeba Timu yao iliyopokonywa Makombe

    ReplyDelete
Previous Post Next Post

International news