FCS yatoa ruzuku ya Bilioni 4/- kwa AZAKI nchini

NA MWANDISHI WETU

SHIRIKA la Foundation for Civil Society (FCS) limetoa ruzuku ya Shilingi shillingi 3,957,301,580 sawa na Bilioni nne (4) kwa asasi za kiraia (AZAKI) 89 Tanzania bara na visiwani kutekeleza miradi ya kimaendeleo chini ya programu za utawala bora katika sekta za maji, elimu, afya na kilimo; usawa wa kijinsia; ujumuishwaji wa vijana na watu wenye ulemavu, na ujenzi wa amani na mshikamamo wa kijamii kwa mwaka 2022-2023.
Wawakilishi kutoka asasi za kiraia wakionyesha mikataba ya ruzuku baina yao na FCS katika mkutano wa mafunzo ya usimamizi wa ruzuku Jijini Dodoma.

Akizungumza katika warsha ya usimamizi wa ruzuku kwa AZAKI hizo zilizochaguliwa kupata ruzuku jijini Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Francis Kiwanga amesema FCS imejitika katika kuhakikisha miradi inayofadhiliwa inawasaidia wananchi katika kuboresha maisha yao na kukuza sekta ya asasi za kiraia.

'’FCS imepitisha mpango mkakati mpya wa mwaka 2022-2026 ambao unataka kuona wananchi waliowezeshwa, wastahimilivu, wanaowajibika na wanaopata haki za kiuchumi, kijamii na kuboresha ubora wa maisha yao. Tutaweza kufanikisha malengo yetu kwa kuchangia maendeleo endelevu na shirikishi nchini Tanzania kwa kuimarisha uwezo, kugawana rasilimali, na ushirikiano wa kimkakati na AZAKIi, vikundi vya jamii pamoja na watendaji wengine wa maendeleo,’’ amesema.
Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Francis Kiwanga (wa kwanza kulia) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya pesa za Kitanzania Shilingi Billioni 3,957,301,580 kwa asasi za kiraia (AZAKI) 89 Tanzania bara na visiwani katika hafla iliyofanyika Leo Agosti 15,2022 Jijini Dodoma.

Edna Chilimo Meneja Programu Utawala Bora FCS alizugumzia ruzuku mbalimbali ambazo FCS imetoa kwa AZAKI ikiwemo ruzuku ndogo, za kati na ruzuku za kimkakati. Alieleza zaidi na kusema,‘

Tunafanya kazi na mashirikia madogo sana ambao wabia wanafika na pia tunafanya kazi na viongozi wa klasta za programu wambao wanafanya kazi katika ngazi ya taifa. Tunafanya kazi na asasi za Kijiji, kata na wilayani.
Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Francis Kiwanga akizungumza wakati wa warsha ya usimamizi wa ruzuku kwa AZAKI zilizochaguliwa kupata ruzuku ya kutekeleza miradi ya kimaendeleo iliyofanyika Leo Jijini Dodoma.

Wabia na mashirika tunayofadhili ni wadau muhimu ili wawafikie wananchi waweza kuleta mabadiliko na maendeleo . Mashirika yanayofadhiliwa na FCS sio Waruzukiwa tu, ni wabia pia.

Baadhi ya Misingi ya ubia ni uelewa wa pamoja,malengo ya pamoja, na kuaminiana ili tuweze kufikia malengo ya pamoja. Tunajengea uwezo Azaki ili ziweze kutekeleza miradi vizuri,kuweza kujiongoza, iwe imara na inayotambulika.
Meneja Programu Utawala Bora, FCS Edna Chilimo alizugumzia ruzuku mbalimbali ambazo FCS imetoa kwa AZAKI katika warsha hiyo.

Tunajengea uwezo Azaki ili kuweza kuandaa na kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Serikali, Sekta binafsi, Mwananchi na Azaki nyingine.

Tumekuwa Walezi wa sekta ya AZAKI. Tumechangia ukuaji wa sekta, miaka ya nyuma tulitoa fedha kwa Azaki kujisajili na sasa kuna Azaki zimekua, kutoka shirika dogo hadi kuwa mashirika makubwa yenye sifa.

“Maadui wakubwa watatu wa maendeleo ni Umaskini, ukosefu wa haki (injustice), hali ya kutenga na kubagua wengine.
Baadhi ya wadau wa asasi za kiraia wakiwa kwenye warsha hiyo Jijini Dodoma.

Mdau mkubwa na maendeleo ni Mwananchi mwenyewe aliyewezeshwa ,anaejitambua, wenye ustaimilivu na mwenye sauti ili aweze kuleta maendeleo yake

”FCS ni shirika huru la maendeleo, la Kitanzania lisilolenga kupata faida, ambalo hutoa ruzuku na huduma za kuzijengea uwezo asasi za kiraia nchini Tanzania.

Tangu kuanzishwa kwake miaka 20 iliyopita FCS imechangia kwa kiwango kikubwa katika kuimarisha uwezo wa sekta ya kiraia nchini Tanzania.
FCS imeziwezesha asasi za kiraia chachu ya maendeleo na wananchi kuwa mstari wa mbele katika kuimarisha utawala wa kidemokrasia nchini Tanzania. Juhudi hizi zinalenga kuboresha utoaji wa huduma, hasa katika ngazi za chini za jamii na hatimaye kuboresha maisha kwa wote.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news