Gethsemane Group Kinondoni SDA yatoa video ya wimbo mpya

NA DIRAMAKINI

KWAYA maarufu nchini ya Gethsemane Group Kinondoni SDA imetoa video ya wimbo wake mpya unaoitwa Nitengeneze Upya Bwana ikiwa ni muendelezo wa kwaya hiyo kutoa nyimbo za kumsifu na kumuabudu Bwana.
Taarifa iliyotolewa na uongozi wa kwaya ya Gethsemane Group Kinondoni jijini Dar es Salaam umesema wimbo kwa sasa umeshazinduliwa na unapatikana kwenye mitandao yao ya kijamii.
“Tumetoa wimbo mpya unaoitwa Nitengeneze Upya Bwana na tayari unapatikana youtube kwenye channel yetu. Kupata channel, ingia youtube na kuandika Gethsemane Group Kinondoni SDA na wataona wimbo lakini pia utakua unapigwa kwenye vyombo vya Habari vyote
“Tunafahamu wapo ndugu zetu ambao watataka kufahamu Wimbo wetu unatoa ujumbe gani ,tunaomba tueleze ujumbe uliomo kwenye wimbo huu ni unyenyekevu mbele za Mungu.Umetungwa kwa kuzingatia kwamba kama wanadamu kuna mara nyingi tunamkosea sana Mungu.

“Hivyo ni wimbo ambao ni ombi la kumuomba Mungu kuendelea kufinyanga na kutengeneza upya mioyo yetu hata pale tunapokosea au kutenda dhambi sana. Kwa kuwa Mungu siku zote ni Mungu wa huruma.
“Tuna imani wimbo huu utaendelea kuleta Watu Karibu na Mungu hata pale wanapojihisi ni wadhambi sana,”umesema uongozi wa kwaya hiyo ambayo imejizolea umaarufu kutokana na aina ya ujumbe unatolewa kupitia nyimbo zake mbalimbali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news