Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo Agosti 21,2022

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachawene amesema ameiona video fupi inayozunguka mitandaoni ikimuonesha kijana akiwajibu vibaya polisi baada ya kutenda kosa la usalama barabarani ambapo amekiri kuwa huyo ni Kijana wake lakini ametaka ashughulikiwe kwa mujibu wa sheria bila huruma.

Kwenye video, kijana huyo licha ya kutenda kosa la usalama barabarani ikiwemo la kuyagonga magari ya Watu, anasikika akitoa kauli mbaya kwa Askari huku akijinasibu kuwa yeye ni Mtoto wa Waziri Simbachawene na hakuna wa kumfanya chochote.

“Nimeiona clip inayozunguka kwenye mitandao ya kijamii, nakiri kuwa huyo ni Kijana wangu ambae ni mtu mzima anajitegemea na ana Familia yake, nimemuagiza Mkuu wa Kituo kwasababu amekosa adabu kwa Jeshi la Polisi na ametenda kosa la usalama barabarani, ashughulikiwe bila huruma kwa mujibu wa sheria.

“Binafsi naomba radhi sana kwa walioathirika na mkasa huo lakini pia kwa Jeshi la Polisi na Watanzania wote poleni kwa usumbufu wowote mlioupata,"ameeleza Mheshimiwa Waziri.


Post a Comment

0 Comments