UKARABATI UWANJA WA MPIRA WA MAJALIWA WAFIKIA ASILIMIA 98

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ukarabati mkubwa uliofanyika kwenye uwanja wa Mpira wa Miguu wa Majaliwa uliopo Ruangwa mkoani Lindi umekamilika kwa asilimia 98 na utakuwa tayari kutumika kwa mechi za Ligi kuu Tanzania Bara.
Muonekano wa Uwanja wa Majaliwa ulipo Ruangwa Mkoani Lindi ambao umefikia asilimia 98 ya maboresho baada matengenezo yake.

Majaliwa amewashukuru wananchi wa Ruangwa kwa kukubali kuchangia shilingi 20/-, kwa kila kilo ya mazao waliyouza ambayo imewezesha Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kukusanya kiasi cha milioni 200 zilizowezesha kununua nyasi bandia.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua uwanja wa Majaliwa baada ya kukamilika kwa sehemu kubwa ya maboresho ya uwanja huo, Ruangwa Mkoani Lindi Agosti 19, 2022. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telak na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hassan Ngoma.

Amesema hayo Agosti 19, 2022 wakati akikagua maendeleo ya ukarabati wa uwanja huo ambao umejengwa kwa viwango vya kimataifa, wilayani Ruangwa mkoani Lindi.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wakazi wa Ruangwa Mkoani Lindi, wakati alipokagua uwanja wa Majaliwa ambao umefikia asilimia 98 ya maboresho baada matengenezo yake.

“Hakuna maendeleo yanayoweza kupatikana mahali bila wewe mwenyewe kuwa msitari wa mbele, wana Ruangwa nyie mmefanya maamuzi mazuri, siyo tu kwenye uwanja bali kwenye maeneo mengi na kwa kweli mmepata mafanikio. Hongereni sana.”

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amewapongeza viongozi wa Halmashauri hiyo kwa kusimamia ukarabati huo ambao utaleta tija kwa timu ya Namungo pamoja na timu nyingine za Mkoa wa Lindi.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia nguzo ya goli wakati alipokagua uwanja wa Majaliwa uliopo Ruangwa Mkoani Lindi, ambao umefikia asilimia 98 ya maboresho baada matengenezo yake

Awali akitoa taarifa ya ukarabati huo, Mhandisi wa viwanja kutoka kampuni ya Azam, Bw. Victor Ndozelo amesema uwanja huo utakapokamilika kwa asilimia 100 utakuwa moja kati ya viwanja bora nchini na tayari wameandaa utaratibu wa kuomba kibali kutoka kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini na lile la soka Barani Afrika (CAF) ili pia uwanja huo uweze kutumika kwa michezo ya kimataifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news