Lifahamu Soko Kuu la kisasa la Njombe Mji linalozinduliwa leo na Rais Samia

HUU ni muonekano wa Soko Kuu la Kisasa la Njombe Mji mkoani Njombe lenye ukubwa wa mita za mraba 9,186.
Soko hili lina sakafu (floors) tatu. Soko lina mifumo na sehemu mbalimbali yakiwemo maduka 162, meza za biashara 407, vyoo 47, migahawa miwili, stoo sita, vizimba vya kuku 27, machinjio ya wanyama wadogo,
Sehemu za huduma za kibenki mbili, ofisi za utawala mbili, mfumo wa maji safi na maji taka, kisima kirefu cha maji.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), pia, soko lina tenki la maji la ardhini lenye ujazo wa lita 500,000 pamoja na pampu ya kupandisha maji, mfumo wa kutambua viashiria vya majanga ya moto (fire detector system).

Mfumo wa kupambana na majanga ya moto (Fire fighting system), Mfumo wa kamera za kiusalama (CCTV Camera system); Mfumo wa habari na mawasiliano (Data and Voice system/PA System) na sehemu za maengesho ya magari yapatayo 120 kwa wakati mmoja.
Aidha, kwa mujibu wa michoro ya usanifu soko lilipangwa kuhudumia wafanyabiashara wasiopungua 630 na limegharimu thamani ya shilingi Bilioni 10.2

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news