Madaraka Nyerere avalishwa medali ya heshima na SADC


Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo akimpongeza Madaraka Nyerere, mwakilishi wa familia ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Kwanza wa Tanzania mara baada ya kuvalishwa medali.Hii ni kama heshima ya kutambua mchango wake katika jumuiya hiyo. Hafla ya utoaji wa medali hizo imefanyika kwenye Mkutano wa 42 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC, Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo tarehe 17 Agosti, 2022.(Picha na Ikulu).

Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa akimvalisha Medali Madaraka Nyerere Mwakilishi wa Familia ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa kwanza wa Tanzania na mmoja wa Waanzilishi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC.

Post a Comment

0 Comments