Makamu wa Rais Dkt.Mpango afungua Maonesho ya Nanenane Kitaifa 2022

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Anthony Mavunde mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya kufungua maonesho ya Nanenane 2022 leo tarehe 1 Agosti 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango leo tarehe 1 Agosti 2022 akifungua Rasmi maonesho ya Nanenane 2022 yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya. Kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dkt. Rashid Chuachua na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi Fredy Mwakibete, Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu na Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Dkt. Geofrey Mkamilo juu kutumia tafiti kuinua mazao mbalimbali nchini ikiwemo zao la parachichi katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dodoma wakati akitembelea Banda la Wizara ya Kilimo katika Maonesho ya Nanenane 2022 yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya leo tarehe 1 Agosti 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimsikiliza mjasiriamali kutoka mkoani Njombe,Upendo Share ambaye ni mfugaji wa Samaki kwa kutumia vitalu nyumba wakati alipotembelea Banda la Halmshauri ya Njombe Mji katika Maonesho ya Nanenane 2022 yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya leo tarehe 1 Agosti 2022.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akitoa maelekezo kwa viongozi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati alipotembelea Banda la Wizara hiyo na kujionea ufugaji wa Samaki katika mabwawa wakati wa maonesho ya Nanenane 2022 yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya leo tarehe 1 Agosti 2022.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akitembelea Mabanda mbalimbali wakati wa Ufunguzi wa maonesho ya Nanenane 2022 yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya leo tarehe 1 Agosti 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza Mkurugenzi wa Ranchi ya Mbogo Pirmohamed Mulla wakati alipotembelea banda la Ranchi hiyo katika maonesho ya Nanenane 2022 yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya leo tarehe 1 Agosti 2022.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news