Mchungaji Sambaya:Kanisa haliwezi kuwa maskini

NA ADELADIUS MAKWEGA

WAKRISTO wamehamasishwa kushiriki kutoa michango mbalimbali ya kanisa, kwani haiwezekani kanisa kuwa fukara na maskini wakati lina watu waliojaliwa watoto, waliojukuu na hata kupata vitukuu huku wengine wakishindwa hata kuwabeba migogoni watoto hao, hiyo ikiwa ni neema kutoka kwa Mungu.
Kauli hiyo imetolewa na Mchungaji Frank Sambaya alipokuwa akitoa mahubiri ya kuhamasisha kuchangisha fedha za ununuzi wa vyombo vya kwaya ya Mtakatifu Grace katika Kanisa la Mtakatifu Luka Chididimo-Ihumwa, Dayosisi Centra Tanganyika mkoani Dodoma iliyofanyika katika viwanja vya kanisa hilo mara baada ya ibada ya asubuhi ya Jumapili ya Julai 31, 2022 kumalizika.
“Kwa kuwa Mungu ametupa baraka tele anataka tumtolee, sasa kiwango cha utoaji kiwaje? Mtu atoe kwa moyo wa kupenda, uoneshe upendo wako kwa kutoa kwa moyo wote, toa kwa ukarimu, usitoe kwa kulazimishwa, ukitoa kwa moyo kazi ya sadaka yako ni kufungua mbingu na hapo baraka zitaongezeka,”amesema Mchungaji Sambaya.

Mchungaji Sambaya aliongeza kuwa, Mungu huwa anatoa vipawa vyake, lakini ujuzi ni jambo la kusomea na ndiyo maana tunakwenda shuleni kusomea ujuzi wa aina mbalimbali.
Mara baada ya mahubiri hayo kwaya mbalimbali za kanisa la Angilikana kutoka dayosisi hiyo ziliimba kuisindikiza kwaya Mtakatifu Grace huku uchangiaji ukifanyika ambapo zilipatikana karibu shilingi milioni 4, lengo likiwa ni shilingi milioni 11 kukamilisha ununuzi wa vifaa vyote vya kwaya hiyo.Harambee hiyo iliwakutanisha watu zaidi ya 200 kutoka maeneo kadhaa ya Jiji la Dodoma na viunga vyake wakitokea taasisi mbalimbali binafsi na umma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news