Mastaa Bongo watembea kifua mbele kuhusu Sensa, watoa wito kwa WATANZANIA

MBWANA GABRIEL CYPIRIAN

Mbwana Gabriel maarufu 'Charles Baba' mwanamziki ambaye ni kiongozi Mkuu wa Twanga Pepeta Sugu Kisima cha burudani amesema, Sensa ni muhimu kwa maendeleo ya Watanzania katika kuiwezesha Serikali kuwa na Takwimu sahihi ya idadi ya wananchi ili kuweza kuwahudumia.

"Naishukuru Serikali ya Tanzania kuleta sensa kwa maana ya kujua idadi ya wananchi wake waliopo ili kurahisisha kutoa huduma ambayo imekamilika kwa idadi ya watu. Unapohesabiwa ndipo unaingia katika hesabu ya Serikali yako.

"Kwa maana tukijulikana tuko wangapi ndio Serikali itajua ijenge hospitali ngapi, kupata matibabu kwa wakati, wanafunzi wako wangapi, madarasa yaongezwe mangapi, tutapaje madawa hospitalini kwa wingi wetu."

"Kwa hiyo mimi ninaomba nikushauri Mtanzania mwenzangu tuwape ushirikiano makarani wa sensa wanaopita katika kaya zetu. Sensa sio vita haina shida, ni kwamba unatakiwa upate maendeleo kupitia sensa. utahudumia vipi familia yako bila kujua mko wangapi.

"Kwa hiyo Mama yetu Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anataka kujua idadi ya wananchi wake ili aweze kutupa huduma iliyo sahihi kwa hiyo Mtanzania mwenzangu tuhesabiwe wote. Mimi Charles Baba tayari nimeshahesabiwa, tuhesabiwe sasa," amesema Charles Baba.

BABU ZEMBWELA


Kwa upande wake Babu Zembwela amesema kuwa, Sensa imempa ushujaa na kujiamini kama Mtanzania sehemu yoyote ndani na nje ya nchi baada ya kuhesabiwa.

"Natembea kifua mbele nikiitwa Mtanzania sehemu na taifa lolote, nami nashukuru sensa ni mmoja kati ya waliohesabiwa.

"Katika muda huu uliobaki wewe ni mmoja kati ya wale mnapaswa kuhesabiwa tuwape ushirikiano makarani wanaopita kuhesabu katika maeneo yetu. Niwape pongezi sana wale wote walioandaa hili zoezi la sensa.

"Mimi niliwaza sana hili labda ni bonge la jambo kubwa sana, kwamba nitaulizwa maswali mazito utani umekuwa mwingi mtandaoni, lakini nilipokutwa na wataalam (makarani) wenyewe wa sensa maswali ni mepesi na yanajibika kirahisi sana.

"Pongezi kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa Watanzania wote ambao wamekubali kwa dhati kuhesabiwa Sensa ni kwa manufaa yetu sote na taifa letu, mimi mwenyewe Zembela nimekubali kuhesabiwa,"amesema Zembwela.

SEIF KISAUJI

Seif Kisauji amesema kuwa, yeye tayari amekwishahesabiwa hivyo ametoa rai kwa wananchi ambao bado hawajahesabiwa kuwa tayari kutoa ushirikiano wa dhati kwa Makarani wa sensa ili wahesabiwe wanapofikiwa katika kaya zao.

"Mimi nimefarijika kwa kuhesabiwa, makarani wamekuja nikajua ni kazi nzito kumbe ni laini, sasa hivi wanavishikwambi tu zamani sisi ili kuwa we acha tu.... Tuwape ushirikiano makarani wetu kwa kutusababisha sisi watujue tuko wangapi kusudi Serikali itupe huduma husika muhimu.

"Niwaombe Watanzania wenzangu kuanzia sasa zimebaki siku chache sana tuhesabiwe wote mimi niseme kwamba nimekwisha hesabiwa. Ninaamini Serikali haitapata tabu mkiwapa ushirikiano hata katika familia yako nyumbani ukijua una idadi ya watu wangapi ni rahisi kuihudumia mkumbuke sensa hii ni kwa faida yetu wenyewe, tuishukuru Serikali kwa kutuletea hii sensa. Sensa kwa maendeleo yetu sote tuhesabiwe naipenda Tanzania,"amesema Seif Kisauji.

VINCENT KIGOSI (RAY)

Msanii maarufu wa filamu hapa nchini, Vincent Kigosi (Ray) amesema anaishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufanya uamuzi wa Sensa ya Watu na Makazi kwani ni muhimu kwa maendeo yetu.

"Hata mwenyewe ukiwa na familia yako huwezi kununua unga ama sukari ama mchele mpaka ujue familia yako ikoje. Mimi Mwenzenu nimeshahesabiwa." amesema Kigosi na kuongeza kuwa.

"Msipotoshwe maswali eti ni magumu ni mepesi sana, karani anakuja na kishikwambi anafanya kazi yake kwa ufanisi. Sensa ni kwa maendeleo ya taifa letu," amesema Vincent Kigosi.

GIFT STANFORD

Gift Stanford maarufu 'Gigy Money' amesema yeye tayari amehesabiwa katika sensa ya watu na Makazi ambayo inaendelea nchini, huku akitoa rai kwa wote ambao bado hawajahesabiwa kuwa tayari kuhesabiwa bila kupitwa kwani ni muhimu kwa maendeleo yao na maendeleo ya nchi.

"Ndugu yangu, Kaka yangu, dada yangu Baba yangu hivi umehesabiwa?, Mimi nimeshahesabiwa juzi tu hapa yaani sensa ni kwa maendeleo yako." amesema Gigy Money.

"Makarani hawana maswali magumu wako very humble (wanyenyekevu)teknolojia imeenda mbele wanatumia vishikwambi kwa wepesi na ufanisi tuhakikishe tunawapa ushirikiano makarani wetu."

"Sensa ni kwa ajili ya Maendeleo yetu taifa zima, ni kwa ajili ya future hakikisha unampa ushirikiano karani unahesabiwa. Hakikisha sensa hii haikupiti ni haki yako unahesabiwa." amesema Gigy money.

NDUMBAGWE MISAYO (THEA)

Msanii katika Tasnia ya Uigizaji Filamu hapa nchini Ndumbagwe misayo maarufu (Thea) amesema yeye tayari amehesabiwa katika zoezi la sensa ya watu na makazi linaloendelea nchini huku akipongeza serikali kufanya zoezi hilo la sensa kisasa zaidi.

"Nichukue fursa hii kuwapongeza watu wote waliohusika na suala zima la sensa, kiukweli limeenda kisasa sana. Kwa sababu nilivyokuwa nikisikia sensa nilikuwa najua inahitaji elimu kubwa sana."

"Lakini kumbe sio, kumbe mtu yeyote anaweza kujibu maswali ya karani yanayoulizwa kirahisi sana. Niwaombe wale ambao hawajahesabiwa makarani watafika Nyumbani (kwenye kaya) kwako onesha ushirikiano kwao kusudi uhesabiwe."

"Sensa ni kwa ajili ya taifa letu na maendeo yetu. Mimi msanii wako mpendwa Thea nimeshahesabiwa." amesema Thea.

DUMA ACTOR

Msanii na Muigizaji maarufu wa Filamu
hapa nchini Duma Marco (Duma Actor)amewataka mashabiki wake na Watanzania wote ambao hawajahesabiwa kuhakikisha wanahesabiwa kama ambavyo yeye amehesabiwa katika zoezi la sensa ya watu na Makazi linaloendelea kufanyika nchi nzima.

Amesema makarani wa sensa watakapowafikia wahakikishe wanatoa ushirikiano wote unaohitajika ikiwemo kutoa taarifa zao kwa usahihi na kujibu maswali yote watakayoulizwa.

"Ni wakati wa kuwapa ushirikiano makarani wa sensa,ni wakati wa kuhesabiwa wewe kama Mtanzania nikwambie tu ni sehemu rahisi sana hiana ukakasi wowote."

"Makarani wetu wanatembea na vishikwambi hawana maswali mengi magumu dakika tano tu ukiwapa ushirikiano wanafanya kazi yao vizuri Sana."

" Mimi Duma Actor nimehesabiwa kwa nini wewe usihesabiwe? Serikali ipo kwa kutaka kujua idadi yetu ituletee maendeleo na mahitaji yetu yote yanayotuzunguka;

Post a Comment

0 Comments