Oman yavutiwa kuwekeza katika madini ya viwandani,ujenzi hapa nchini

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI ya Oman imevutiwa kuwekeza katika madini ya viwandani na madini ya ujenzi yanayopatikana hapa nchini Tanzania.
Kauli hiyo, ameitoa Balozi wa Oman nchini Tanzania Said All-Shidham baada ya kukutana na Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko katika Ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam.

Balozi Shidham amesema nchi ya Oman imevutiwa kuwekeza kutokana na hali ya utulivu uliyopo nchini, amani, na mazingira wezeshi kwenye Sekta ya Madini chini ya Uongozi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake, Dkt. Biteko amesema milango ya Wizara ya Madini kwa wawekezaji iko wazi na kuwataka wale wote wenye nia ya kuwekeza kwenye Sekta ya Madini nchini Tanzania wafike Wizarani hapo.

Aidha, Dkt. Biteko amesema Wizara ya Madini inawahitaji wawekezaji kuliko wawekezaji wanavyoihitaji Wizara hiyo ambapo amewaomba waje nchini kuwekeza kwenye sekta hiyo.

Pia, Dkt. Biteko amekutana na kuzungumza na Kampuni ya uchimbaji wa madini ya almasi ya Williamson Diamond Limited (DWL) kwa lengo la kupata mrejesho wa kikao kilichofanyika awali.baada ya kukutana na Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko katika Ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam.

Balozi amesema nchi ya Oman imevutiwa kuwekeza kutokana na hali ya utulivu uliyopo nchini, amani, na mazingira wezeshi kwenye Sekta ya Madini chini ya Uongozi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake, Dkt. Biteko amesema milango ya Wizara ya Madini kwa wawekezaji iko wazi na kuwataka wale wote wenye nia ya kuwekeza kwenye Sekta ya Madini nchini Tanzania wafike Wizarani hapo.
Aidha, Dkt. Biteko amesema Wizara ya Madini inawahitaji wawekezaji kuliko wawekezaji wanavyoihitaji Wizara hiyo ambapo amewaomba waje nchini kuwekeza kwenye sekta hiyo.

Pia, Dkt. Biteko amekutana na kuzungumza na Kampuni ya uchimbaji wa madini ya almasi ya Williamson Diamond Limited (DWL) kwa lengo la kupata mrejesho wa kikao kilichofanyika awali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news