Serikali yatoa habari njema, kila halmashauri, mkoa kuwezeshwa magari ya kutolea huduma

NA OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa ma Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa amesema, watapeleka kwenye kila halmashauri gari moja la kubebea wagonjwa pamoja na Hardtop (TOYOTA LAND CRUISER) moja huku mkoani wakipata Hardtop moja kwa ajili ya ufuatiliaji wa shughuli za afya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kama ishara ya kuzindua rasmi Soko Kuu la Njombe Mjini katika hafla iliyofanyika mkoani Njombe leo Agosti 10, 2022.

Amesema, tayari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameshatoa shilingi Bilioni 149.5 kwa ajili ya vifaa tiba na maelekezo ni kila mkoa upate gari aina ya Hardtop moja na kila halmashauri Hardtop moja na gari la kubebea wagonjwa.

"Na mpaka sasa tuko kwenye hatua za manunuzi tukikamikisha tu mtaanza kupokea magari hayo kwenye maeneo yenu;

Mheshimiwa Bashungwa ameyasema hayo leo Agosti 10, 2022 mbele ya Raia Samia Suluhu Hassan wakati wa mkutano wake na wananchi kwenye uwanja wa Sabasaba mkoani Njombe.

Amesema, Mhe.Raia amewawezesha kujenga zahanati, vituo vya afya na hospitali za wilaya kwenye halmashauri zetu.

"Na sasa umetupatia fedha kwa ajili ya vifaa tiba na magari, nikuhakikishie tu kuwa vifaa hivyo tutavipelela kama ulivyoelekeza,"amesema Mheshimiwa Bashungwa.

Ameongeza kuwa, "Wakazi wa Mkoa wa Njombe jiandaeni tu kupokea magari yenu tutakapokamilisha mchakato tu tutayaleta,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news