Prof.Muhongo ahesabiwa na wanakaya yake Musoma Vijijini

NA FRESHA KINASA

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara, Prof. Sospeter Muhongo na wanakaya yake walioamkia nyumbani leo Agosti 23,2022, tayari wahesabiwa.

Mheshimiwa Prof. Muhongo amesema waliohesabiwa ni wanakaya sita na wageni wawili. "Karani anafanya kazi yake kwa weledi mkubwa sana. Wanakaya na wageni wote wamejibu maswali yote kwa usahihi unaotakiwa.

"Watanzania wote tuendelee kuhesabiwa kwa faida yetu na maendeleo ya nchi yetu.Ukweli na takwimu za kuaminika na zisizo na shaka ni hitaji la lazima kwa mipango, bajeti, miradi na programu zozote zinazohitajika, zenye maandalalizi mazuri na misingi imara,"amesema Prof.Muhongo.

Picha za hapa chini zinawaonesha watu nane waliohesabiwa nyumbani kwa Prof.Muhongo. Karani nae yuko pichani.

Post a Comment

0 Comments