Prof.Muhongo ampa tabasamu kijana aliyechelewa shule kwa kukosa mahitaji

NA FRESHA KINASA

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini Mkoa wa Mara, Mheshimiwa Prof.Sospeter Muhongo amemsaidia mahitaji ya shule kijana Jastine Mgaya Bina wa Kijiji cha Kaburabura, Kata ya Bugoji aliyechelewa kuanza masomo ya Kidato cha Tano (Form V, HGL) kwa kukosa mahitaji ya shule yaliyokuwa yakihitajika.

Hayo yamebainishwa leo Agosti 31,2022 kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Mheshimiwa Prof.Muhongo.

"Leo, kijana huyo amepata mahitaji yote ikiwemo vitabu na nauli yake ya kwenda kuanza masomo yake Nyakato High School, Bukoba Mkoa wa Kagera,"imeeleza taarifa hiyo.

Kwa upande wake kijana huyo Jastine Mgaya Bina amemshukuru Mheshimiwa Prof. Muhongo kwa kumsaidia mahitaji yote na vitabu, ambapo amesema atahakikisha anasoma kwa bidii na malengo ili afikie ndoto zake.

Mheshimiwa Prof.Muhongo shauku yake kubwa ni kuona vijana wa Jimbo la Musoma Vijijini na Watanzania kwa ujumla wanasoma na kufika mbali zaidi kielimu kusudi waje wasaidie kusukuma mbele juhudi za Serikali za kuwa na taifa la watu wasomi watakao chagiza kuleta ufanisi wa kimaendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Katika Jimbo la Musoma Vijijini mara kwa mara amekuwa akisaidia vijana ambao hukabiliwa na Changamoto za kiuchumi ambao hufaulu amekuwa akiwawezesha kupata mahitaji yao yote sambamba na kufuatilia maendeleo yao kitaaluma kwa karibu.

Huku akiwahimiza Wazazi na walezi kulipa mkazo suala la elimu kwani linatija kubwa kuanzia ngazi ya familia, Jamii hadi taifa.
Picha iliyoambatanishwa hapa inamuonesha Msaidizi wa Mbunge, Vaileth Peter akiwa na kijana Jastine Mgaya Bina ambao wametoka benki kufanya malipo ya shule, na tayari wamemaliza kununua vifaa vya shule, vikiwemo vitabu vinavyohitajika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news