Qatar yaipa saluti Tanzania kwa kufanikisha Mkutano Mkuu wa 44 wa Kawaida wa CAF

NA GODFREY NNKO

CHAMA cha Mpira wa Miguu cha Qatar (QFA) kimelipongeza Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kufanikisha Mkutano Mkuu wa 44 wa Kawaida wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) uliofanyika Agosti 10, mwaka huu jijini Arusha.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 15, 2022 na Bw.Cliford Mario Ndimbo ambaye ni Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF.

Kwa mujibu wa barua ya Rais wa QFA, Hamad Bin Khalifa Al-Thani kwa Rais wa TFF, Wallace Karia, ameshukuru kwa ukarimu uliooneshwa kwake pamoja na wajumbe wa mkutano huo.

"Nachukua fursa hii kukupongeza wewe binafsi pamoja na wenzako kwa kufanikisha Mkutano Mkuu wa CAF, ni tukio ambalo limewakutanisha watu wa Bara la Afrika kwa ajili ya maendeleo ya mpira wa miguu.

"Mpira wa miguu kwa Afrika mara zote umebakia kuwa mchezo unaowaleta watu pamoja. Hili limethibitishwa na jinsi Mkutano Mkuu wa 44 wa Kawaida wa CAF ulivyoandaliwa,"imesema sehemu ya barua hiyo ya Bin Khalifa Al-Thani, kupitia taarifa iliyotolewa na Afisa Habari na Mawasiliano TFF, Bw.Ndimbo.

Post a Comment

0 Comments