Rais Dkt.Mwinyi afanya uteuzi

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar an Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa viongozi wawili.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Agosti 16, 2022 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said ambapo uteuzi huo unaanza Agosti 16, 2022.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Dkt.Idrissa Muslim Hija kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Ardhi katika Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi.

Dkt.Idrissa kabla ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi alikuwa Mwenyekiti wa iliyokuwa Bodi ya Uhaulishaji wa Ardhi Zanzibar.

Wakati huo huo, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Khamis Juma Khamis kuwa Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Ardhi katika Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi.

Kabla ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Mwinyi, Bw.Khamis alikuwa ni Afisa Sheria Mwandamizi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF).

Post a Comment

0 Comments