Rais Samia aagiza kila mkoa kutenga eneo litakalotumika kwa kilimo

NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameuagiza kila mkoa kutenga eneo litakalotumika kwa kilimo cha mazao yanayozalishwa katika mkoa husika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia uzalishaji wa miche pamoja na bidhaa mbalimbali zitokanazo na kilimo wakati alipotembelea Banda la Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) na Banda la Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa mbegu Tanzania (TOSCI) kwenye kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane Kitaifa ambayo imefanyika katika Viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.

Rais Samia ametoa agizo hilo leo wakati akihutubia kwenye kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya wakulima (Nanenane) iliyofanyika katika uwanja wa John Mwakangale.

Aidha, Rais Samia amewataka wakulima kutumia maeneo hayo yatakayotengwa kuzalisha kibiashara ili kupata chakula cha kutosha na kuuza kwa nchi jirani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua na kuangalia vifaa mbalimbali vya shughuli za ufugaji wa ng’ombe vilivyopo katika banda la Asas kwenye kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane Kitaifa ambayo imefanyika katika Viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.

Vile vile, Rais Samia amewataka wakulima kujisajili ili kupata vitambulisho ambavyo vitatumika kupata ruzuku ya mbolea kuendana na misimu.

Rais Samia pia amemuelekeza Waziri wa Mifugo na Uvuvi kushirikiana na Chuo cha Kilimo (SUA) ili kuwezesha vijana wanaohitimu chuoni hapo kuweza kujiajiri katika sekta hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia utiaji saini wa Mikataba ya skimu ya Umwagiliaji, alipotembelea Mabanda ya Wizara ya Kilimo kwenye kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane Kitaifa ambayo imefanyika katika Viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.

Kwa upande mwingine, Rais Samia ameitaka Bodi ya Wakurugenzi na Uongozi wa NARCO kufanya uchambuzi wa vitalu vya ranchi vilivyokodishwa na kujua mapato yatokanayo na vitalu hivyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi Mfumo wa ruzuku ya Mbolea mara baada ya kutembelea Mabanda na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na wadau wa Kilimo kwenye kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane Kitaifa ambayo imefanyika katika Viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhi mfano wa funguo za Trekta kwa ajili ya wakulima bora ambao wamepewa zawadi kutokana na mafanikio waliyopata katika kilimo kwenye kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane Kitaifa ambayo imefanyika katika Viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.

Halikadhalika, Rais Samia ameiagiza Wizari ya Mifugo na Uvuvi kufuta leseni za vitalu vilivyokodishwa na kupanga upya ili kufanya uwekezaji wenye tija.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news