Rais Samia afanya uteuzi

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi wa taasisi mbili.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Bi.Zuhura Yunus leo Agosti 15,2022 ambapo uteuzi huo umeanza Agosti 11, 2022.

Kwa mujibu was taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Samia amemteua Bw. Binilith Satano Mahenge,mkuu wa mkoa wa Singida mstaafu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Mheshimiwa Mahenge anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof.Longinus Tutasitara ambaye amemaliza muda wake.

Wakati huo huo, Mheshimiwa Rais Samia amemteua Prof.Aurelia Kokuletage Ngirwa Kamuzora ambaye ni Profesa Mshiriki wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Prof. Kamuzora anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt.Festus B.Limbu ambaye alimaliza muda wake.

Post a Comment

0 Comments