Rais Samia afunga Mafunzo ya Awali ya Askari 818 wa Jeshi la Uhamiaji

Rais wa Jamhuri ya Muunno wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Salaam na Wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Jeshi la Uhamiaji Boma Kichakamiba Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga kwa ajili ya kufunga Mafunzo ya Awali ya Askari 818 wa Jeshi la Uhamiaji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi na Askari wahitimu wa Mafunzo ya Awali Kozi Na. 1,2022 ya Jeshi la Uhamiaji pamoja na Wananchi katika Hafla ya Ufungaji wa Mafunzo hayo iliyofanyika katika Chuo cha Uhamiaji Boma Kichakamiba Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria kuweka Jiwe la Msingi wa Ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Jeshi la Uhamiaji Boma Kichakamiba Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipanda mti mbele ya Jengo la Ofisi za Chuo cha Jeshi la Uhamiaji Boma Kichakamiba Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga, alipowasili Chuoni hapo kwa ajili ya kufunga Mafunzo ya Awali ya Askari 820 wa Jeshi la Uhamiaji.
Askari wa Mafunzo ya Awali ya Jeshi la Uhamiaji Kozi Na. 1,2022 wakila kiapo cha Utii mbele ya Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwenye Hafla ya ufungaji wa Mafunzo hayo yaliyofanyika katika Chuo cha Uhamiaji Boma Kichakamiba Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikabidhi Cheti kwa Mshindi wa Jumla kwenye Mafunzo ya Awali Kozi Na. 1,2022 ya Jeshi la Uhamiaji Konstebo Geofrey Felician Zakaria, wakati wa Ufungaji wa Mafunzo hayo yaliyoshirikisha jumla ya Wahitimu 818 katika Chuo cha Boma Kichakamiba Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Hamad Masauni kabla ya kufungua Mafunzo ya Awali Kozi Na. 1,2022 ya Jeshi la Uhamiaji katika Hafla iliyofanyika Chuo cha Uhamiaji Boma Kichakamiba Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news