RC Makongoro Nyerere ahesabiwa na familia yake nyumbani Mjini Babati

NA DIRAMAKINI

MKUU wa Mkoa wa Manyara, Charles Makongoro Nyerere leo tarehe 23 Agosti 2022 ameshiriki zoezi la Sensa ya Watu na Makazi,akihesabiwa yeye na familia yake katika makazi yao mtaa wa Mrara Mjini Babati.
Akizungumza mara baada ya kushiriki zoezi hilo, Nyerere ametoa rai kwa wakazi wa mkoa wa Manyara kutoa ushirikiano kwa makarani wa sensa pindi wanapofika Katika maeneo yao ili waweze kupata taarifa sahihi zitakazoisaidia serikali kupanga vyema maendeleo.

Amesema zoezi la sensa ni wajibu wa kila mtanzania hivyo inapaswa kufanywa kwa uadilifu mkubwa.

Aidha amesema amefurahishwa na maswali yanayoulizwa katika zoezi la sensa ya watu na makazi ambayo yanalenga huduma muhimu za kijamii zinazopatikana katika maeneo ya wananchi ili kuiwezesha serikali kutambua huduma zinazokosekana katika maeneo hayo na uhitaji wake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news