Ruvu Shooting yang'ara kwa Ihefu FC, Namungo na Mtibwa Sugar zatoshana nguvu

NA DIRAMAKINI

KIPENGA cha Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kimepulizwa rasmi, huku Ruvu Shooting ya mkoani Pwani ikianza vema msimu mpya.

Ni baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Ihefu FC ya mkoani Mbeya kupitia mtanange uliopigwa katika dimba la Highland Estate lililopo Ubaruku wilayani Mbarali mkoani humo.

Mtanange huo wa Agosti 15, 2022 bao pekee la Ruvu Shooting limefungwa na nyota wake, Ally Bilal dakika ya 19 ya mchezo huo. Kwa matokeo hayo Ruvu Shooting tayari ina mtaji wa alama tatu za mwanzo.

Wakati huo huo,Namungo FC ya mkoani Lindi imelazimishwa sare ya 2-2 na Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro katika mchezo wa ligi hiyo.

Ni kupitia mtanange uliopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Lusajo Mwaikenda dakika ya 32 na 82 ndiye aliyewapa raha wana Namungo kwa mabao yote huku upande wa Mtibwa Sugar yakifungwa na Vedastus Mwihambi dakika ya 55 na Nickson Kibabage dakika ya 80 ya mchezo huo.

Kupitia mtanange huo, Namungo FC huenda wakajutia kwa kupoteza alama tatu baada ya nyota wao, Kassim Haruna kukosa penalti kipindi cha pili ya mtanange huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news