NA MWANDISHI WETU
SERIKALI kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeahidi kushirikiana na Hospitali ya CCBRT kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma za afya nchini kupitia utekelezaji wa Diplomasia ya Afya.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akioneshwa baadhi ya viungo bandia vinavyotengenezwa katika hospitali ya CCBRT na Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBT, Bibi. Brenda Msangi. Balozi Mulamula alifanya ziara ya kutembelea hospitali hiyo kwa lengo la kujionea shughuli na huduma zinazotolewa hospitalini hapo leo Jijini Dar es Salaam.
Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb.), alipofanya ziara ya kutembelea Hospitali hiyo kwa lengo la kujionea shughuli na huduma mbalimbali zinazotolewa hospitalini hapo leo Jijini Dar es Salaam
Pamoja na mambo mengine, Waziri Mulamula ameupongeza Uongozi wa Hospitali hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuwahudumia watanzania hasa kuwapa akina mama tumaini la maisha hususan wanaopatwa na changamoto ya ugonjwa wa fistula.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga akieleza jambo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBT, Bibi. Brenda Msangi hospitalini hapo leo Jijini Dar es Salaam.
“Wizara ninayoisimamia ni mtambuka na mchango wake umekuwa mkubwa ambapo nyinyi ni wadau wetu, tutashirikiana na Balozi zetu nje kuona ni jinsi gani tutapata wadau/washirika wa maendeleo watakaosaidia katika kuboresha sekta ya afya hususan hapa CCBRT,” amesema Waziri Mulamula.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika kikao na Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBT, Bibi. Brenda Msangi wakati alipofanya ziara ya kutembelea hospitali hiyo kwa lengo la kujionea shughuli na huduma zinazotolewa hospitalini hapo leo Jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBT, Brenda Msangi amesema kuwa pamoja na jitihada ambazo Serikali imekuwa ikizichukua kuboresha sekta ya afya nchini, hospitali hiyo pia inajitahidi kuboresha huduma zake na mazingira yake kwa ujumla ili kuweza kuwahudumia wagonjwa wengi zaidi.
“Tunajitahidi kuwahudumia watanzania kadri tuwezavyo ila tunakabiliwa na baadhi ya changamoto za msaada wa utoaji wa huduma, vifaa tiba pamoja na kuwajengea uwezo wataalamu wetu ili kuweza kuboresha huduma zaidi,” amesema Bibi. Msangi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiongea na baadhi ya wagonjwa wakati alipofanya ziara ya kutembelea hospitali ya CCBRT kwa lengo la kujionea shughuli na huduma zinazotolewa hospitalini hapo leo Jijini Dar es Salaam.
Julai 5, 2022 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa jengo la kutolea huduma ya afya ya mama na mtoto katika hospitali ya CCBRT alisema kuwa mikakati ya kuboresha huduma kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga, Serikali kupitia Wizara ya afya kwa kushirikiana na vyama vya kitaaluma vya madaktari bingwa wa magonjwa ya kina mama na uzazi wameanzisha mfumo wa kupitia takwimu za vifo vya kina mama na watoto wakati wa kujifungua lengo likiwa ni kuboresha zaidi huduma katika sekta ya afya.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga akiagana na Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBT, Bibi. Brenda Msangi hospitalini hapo leo Jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBT, Bibi. Brenda Msangi akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula wakati Mhe. Mulamula alipofanya ziara ya kutembelea hospitali hiyo kwa lengo la kujionea shughuli na huduma zinazotolewa hospitalini hapo leo Jijini Dar es Salaam.