Rais Dkt.Mwinyi ateua viongozi mbalimbali leo Agosti 10, 2022

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameteua viongozi mbalimbali leo.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 10, 2022 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said ambapo uteuzi huo unaanza leo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, walioteuliwa ni Juma Burhan Mohamed kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar katika Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji.

Bw. Mohamed kabla ya uteuzi huo alikuwa Meneja wa Benki ya Diamond Trust tawi la Kijangwani jijini Zanzibar.

Pili, kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Waheed Muhammad Ibrahim Sanya kuwa Msajili wa Hazina katika Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango.

Kabla ya uteuzi huo,Waheed alikuwa ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA). Pia Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Bibi Mtumwa Khatib Ameir kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA) katika Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi.

Bibi Mtumwa ni Afisa Msimamizi Mkuu wa Haki Miliki za Wasaniii Zanzibar (COSOZA). Uteuzi wa nne, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Bw.Abdulhalim Mohammed Mzale kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa katika Wizara ya Afya Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kabla ya uteuzi huo Bw. Abdulhalim alikuwa Afisa Mwandamizi katika Hospitali ya Global.

Aidha, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Hidaya Juma Hamad kuwa Mfamasia Mkuu wa Serikali katika Wizara ya Afya. Kabla ya uteuzi huo, Hidaya alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Mashirikiano ya Masuala ya Madawa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kupitia Wizara ya Afya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news