Simba Queens yagawa dozi CECAFA

NA DIRAMAKINI

KIKOSI Simba cha Timu ya Wanawake cha Simba Queens kimeanza vema michuano ya Ligi ya Mabingwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) baada ya kugawa dozi kwa Garde Publicaine FC ya Djibouti mabao 6-0.
Simba Queens walianza vyema michuano hiyo baada ya kuichakaza Garde Republicaine ya Djibouti katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Simba Queens katika mchezo huo wa Kundi B yalifungwa na Fallone Pambani, Joelle Bukuru na Asha Djafar mawili kama Olaiya Barakat.

Mchezo huo ulikuwa wa upande mmoja zaidi huku Simba Queens wakitawala sehemu kubwa na kufanya mashambulizi mengi.

Fallone Pambani alitupatia bao la kwanza dakika ya 30 kabla ya Olaiya Barakati kuongeza la pili dakika mbili baadae huku Asha Djafar akitupia la tatu na kuwafanya Simba Queens kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 3-0.
Kipindi cha pili walirudi kwa kasi ambapo dakika ya 51 Joelle Bukuru alitupatia bao la nne na Djafar kuongeza la tano dakika ya 68.

Olaiya alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga la sita likiwa na pili kwake katika mchezo huo baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Garde Republicaine ya Djibouti.

Post a Comment

0 Comments