Bodi ya Ligi Kuu Tanzania yataja sababu za kufanya maboresho ratiba Ligi Kuu ya NBC

NA GODFREY NNKO

BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TLP) imefanya maboresho katika ratiba ya Ligi Kuu ya NBC msimua wa 2022/2023.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari an Mawasiliano ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TLB) Agosti 14, 2022 bodi imefikia hatua hiyo kutokana na kufungiwa kwa viwanja vitano huku vingine vitatu vikiwa katika hatua za mwisho za maboresho wakati ligi hiyo ikianza leo.

Mabadiliko hayo yanahusisha michezo miwili iliyobadilishwa tarehe, muda na viwanja, michezo mitatu iliyobadilishwa viwanja na mchezo mmoja uliobadilishwa muda na uwanja.

Kwa mujibu wa TBL, viwanja vilivyosimamishwa kuendelea kutumika kwa michezo ya Ligi Kuu ya NBC ni Mkwakwani (Tanga), Nyankumbu Girls (Geita), Ushirika (Kilimanjaro),Mabatini (Pwani) na Jamhuri jijini Dodoma.

Aidha, viwanja vilivyo kwenye maboresho ni Majaliwa (Ruangwa-Lindi), Sokoine mkoani Mbeya na Kaitaba mkoani Kagera.

Post a Comment

0 Comments