TRA yakusanya Trilioni 22.99/- yaeleza mikakati mipya

NA DIRAMAKINI

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya shilingi trilioni 22.99 na kufikia lengo la asilimia 99.22 ambalo ni ukuaji wa asilimia 22.77 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/22.

Mafanikio hayo yametokana na ushirikiano ulioneshwa na walipa kodi kwa kuitikia wito wa kulipa kodi kwa wakati.
Hayo yamesemwa leo Agosti 12, 2022 na Richard Kayombo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi alipokuwa akizungunza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu ya namna walivyotekeleza majukumu yao mwaka 2021/2022 na mikakati waliyonayo mwaka 2022/2023.

Amesema, mafanikio ya mwaka jana yalitokana na maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa vitendo kwa kukusanya kodi wa weledi, kukaa na walipa kodi, kutatua changamoto zao ikiwemo kuweka mazingira rafiki ya kulipa kodi zao pamoja na kuongeza kasi ya kupanua wigo kwa kusajili walipakodi wapya.

Amesema, katika mwaka wa fedha wa 2022/2023, mamlaka imeanza kwa kuelimisha watumishi wao na wafanyabiashara kote nchini mabadiliko mbalimbali ya sheria za kodi, tozo na ada zinazosimaiwa na TRA na taratibu za ukusanyaji wa mapato ya Serikali.

"Kwa watumishi tunawaelimisha ili wawe na lugha moja katika kuwahudumia wateja, lakini pia walipa kodi tunawaelimisha viwango vya kodi, wakati wa kulipa na namna ya kulipa.

"Lengo kubwa la marekebisho hayo ni kuhakikisha wananchi wote wanakuwa na uelewa mmoja juu ya kodi ili kurahisisha ukusanyaji na ulipaji wake kwa hiari yanayolenga kusaidia kuongeza kasi ya kukufufua uchumi na kuimarisha sekta ya uzalishaji kwa ajili ya kuboresha maisha,"amesema Kayombo.

Ameyataja maeneo yaliyoboreshwa kuwa ni pamoja na kutoa msamaha wa ushuru wa bidhaa kwenye vifungashio vya plastiki vya mboga mboga na maua.

Pia utozaji wa ushuru wa asilimia 10 wa bidhaa kwenye betri za maji zinazotoka nje kwa lengo la kulinda viwanda vya ndani na kwenye sheria ya magari ya kigeni ili kuweka uwiano kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka dola 16 hadi dola 10 kwa kila kilomita 100 ili nchi wanachama wasiogope kutumia bandari yetu.

Kayombo ameongeza kuwa, katika kuzingatia ulipaji Kodi wamefanya madaliko katika sheria ya wapangaji ambapo kwa mpangaji iwe nyumba binafsi au ya biashara anawajibika kuzuia asilimia 10 ya pango ili kuiwasilisha TRA kwani ni jukumu la wapangaji kulipa kodi hiyo.

Ameongeza kuwa kwa kurahisisha ulipaji kodi kwa wafanyabiadhara wadogo. Walipa kodi wanostahili ni wale wa kuanzia mil 4. Lakini wapo wale wadogo kuanzia milioni 11-99 wao watalipa asilimia 3.5 ya mauzo huku mwenye mauzo yanayozidi sh.milioni nne na hayazidi sh.milioni saba malipo yake ya kodi sh. 100,000 ambayo ni asilimia tatu ya mauzo yanayozidi sh. milioni nne.

Kayombo ameongeza kuwa, mkakati wa TRA kwa mwaka 2022/2023 ili kufanikisha lengo la ukusanyaji kodi ni kuongeza usimamizi wa utoaji risiti kwa njia ya EFD na kuziba mianya yote ya udanganyifu.

Sambamba na kukabiliana na vishoka pamoja na matapeli wanaochafua jina la TRA, kukabiliana na magendo kote nchini,kufanya bahati nasibu kubwa ya EFD kuongeza kasi ya kutoa elimu ya kodi kwa makundi mbalimbali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news