Viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Agosti 15,2022

NA GODFREY NNKO

LEO Kwacha ya Malawi (MWK) inanunuliwa kwa shilingi 2.08 na kuuzwa kwa shilingi 2.22 huku Rupia ya Pakistan (PKR) ikinunuliwa kwa shilingi 10.12 na kuuzwa kwa shilingi 10.75.
Picha na mbcheck.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Agosti 15, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Dirham ya Umoja wa Falme za Kiarabu (AED) inanunuliwa kwa shilingi 624.39 na kuuzwa kwa shilingi 630.50 huku Schilling ya Australia (ATS) ikinunuliwa kwa shilingi 147.16 na kuuzwa kwa shilingi 148.46.

Dola ya Zimbabwe (ZWD) inanunuliwa kwa shilingi 0.43 na kuuzwa kwa shilingi 0.44 huku Euro ya Ulaya (EUR) inanunuliwa kwa shilingi 2357.44 na kuuzwa kwa shilingi 2381.24.
Aidha,Paundi ya Uingereza (GBP) inanunuliwa kwa shilingi 2781.45 na kuuzwa kwa shilingi 2809.50 huku Dinar ya Algeria (DZD) ikinunuliwa kwa shilingi 16.59 na kuuzwa kwa shilingi 16.60.

Krona ya Sweden (SEK) inanunuliwa kwa shilingi 225.59 na kuuzwa kwa shilingi 227.80 huku Randi ya Afrika Kusini (ZAR) ikinunuliwa kwa shilingi 141.02 na kuuzwa kwa shilingi 142.39.

Shilingi ya Uganda (UGX) inanunuliwa kwa shilingi 0.58 na kuuzwa kwa shilingi 0.61 huku Franka ya Burundi (BIF) ikinunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21.

Rupia ya India (INR) inanunuliwa kwa shilingi 28.77 na kuuzwa kwa shilingi 29.04 huku Shilingi ya Kenya (KES) inanunuliwa kwa shilingi 19.23 na kuuzwa kwa shilingi 19.39.
Franka ya Rwanda (RWF) inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.25 huku Kwacha ya Zambia (ZMK) ikinunuliwa kwa shilingi 141.27 na kuuzwa kwa shilingi 143.41.

Post a Comment

0 Comments