Waziri Balozi Mulamula apokea nakala za hati za utambulisho za mabalozi tisa

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) amepokea nakala za Hati za Utambulisho za Mabalozi tisa katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam leo Agosti 24 2022.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Jamhuri ya Slovakia nchini, mwenye makazi yake Nairobi Kenya, Katarina Žuffa Leligdonová katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Agosti 2022.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Jamhuri ya Sudan Kusini, Mhe. Loyang Johnson Okot Jekery katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Agosti 2022.

Mabalozi waliowasilisha nakala za hati za utambulisho kwa Mhe. Waziri ni Balozi mteule wa Iran, Mhe. Hossein Alvandi Bahineh, Balozi mteule wa Kenya, Mhe. Isaack Njenga Gatitu, Balozi mteule wa Sweden, Mhe. Charlotta Ozaki Macias. Balozi mteule wa Ubelgiji, Mhe. Peter Huyghebaert, Balozi mteule wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Mhe.Noluthando Mayende-Malepe pamoja na Balozi Mteule wa Jamhuri ya Sudan Kusini,Mhe. Loyang Johnson Okot Jekery.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Ukraine nchini, mwenye makazi yake Nairobi Kenya, Mhe. Pravednyk Andrii katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Agosti 2022.

Mabalozi wengine waliowasilisha nakala za Hati za Utambulisho ambao makazi yao yapo Nairobi, Kenya ni Balozi wa Thailand, Mhe. Sasirit Tangulrat, Balozi wa Ukraine, Mhe. Pravednyk Andrii pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Slovakia, Mhe. Katarina Žuffa Leligdonová.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mteule wa Sweden, Mhe. Charlotta Ozaki Macias katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Agosti 2022.

Mara baada ya kupokea nakala hizo kutoka kwa mabalozi hao, Waziri Mulamula amewapongeza na kuwaahidi kuwa Wizara itawapa Ushirikiano wa kutosha ili waweze kutekeleza majukumu yao ya kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na mataifa hayo kwa ufanisi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mteule wa Ubelgiji, Mhe. Peter Huyghebaert katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Agosti 2022
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mteule wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Mhe. Noluthando Mayende-Malepe katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Agosti 2022.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Thailand nchini, mwenye makazi yake Nairobi Kenya, Mhe. Sasirit Tangulrat katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Agosti 2022.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mteule wa Kenya, Mhe. Isaack Njenga Gatitu katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Agosti 2022.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mteule wa Iran, Mhe. Hossein Alvandi Bahineh katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Agosti 2022.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news